Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Ferguson haamini mwamuzi Clattenburg alitumia lugha isiyofaa kwenye mchezo wao na Chelsea

Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester Unite Sir Alex Ferguson ameweka wazi haamini kama mwamuzi Mark Clattenburg alitumia lugha isiyofaa michezoni na yenye mwelekeo wa kibaguzi kwa Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi. Ferguson amesema kwa upande haamini mwamuzi wa kiwango cha Clattenburg anaweza akatumia lugha ambayo inaelezwa aliitumia katika mchezo baina ya Manchester United na Chelsea uliopigwa jumapili iliyopita.

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa kwenye kikao na waandishi wa habari
Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa kwenye kikao na waandishi wa habari
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Ferguson imekuja kipindi hiki ambacho Chelsea imewasilisha tuhuma zake rasmi kwa Chama Cha Soka nchini Uingereza FA juu ya mwamuzi Clattenburg kutumia lugha isiyofaa kwa wachezaji wake waili Juan Mata na Mikel Obi.

Ferguson kwenye kikao chake na waandishi wa habari kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal ameweka wazi haamini kama mwamuzi anayepatanafasi ya kucheza Ligi kubwa kama ya Uingereza anaweza kuthubutu kufanya hivyo.

Kocha huyo mkongwe amekiri tuhuma za Chelsea dhidi ya Mwamuzi Clattenburg hazifikiriki na kwa upande wake imekuwa vigumu sana kukubaliana na tuhuma hizo akiamini waamuzi wapo makini.

Ferguson licha ya kuonekana kutokuwa tayari kukubalia tuhuma za mwamuzi Clattenburg anaweza akawa ametumia lugha isiyofaa lakini amekiri mchezo wa mpira wa miguu umebadilika sana ukilinganisha na ilivyokuwa miaka 25 iliyopita.

Kocha huyo wa Manchester United amekiri yeye ni miongoni mwa wale ambao wamekuwa wakikosa maamuzi ya Waamuzi lakini hajawahi kufikiria hata mara moja kama wamekuwa wakitumia lugha za kibaguzi kwa wachezaji.

Clattenburg alikutana na tuhuma za kutoa lugha isiyofaa michezoni katika mchezo ambao Chelsea walipata kichapo cha nyumba cha magoli 3-2 kutoka kwa Manchester United huku maamuzi yake yakikosolewa mno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.