Pata taarifa kuu
michezo

Federer ajielekeza katika ubingwa wa michuano ya Paris..

Roger Federer anakabiliwa na kibarua kigumu kuinua ubingwa wake katika msimu wa michuano ya mara kwa mara ya bingwa wa Paris inayoanza kutimua vumbi jumatatu ijayo.

Bingwa wa Tennis Roger Federer
Bingwa wa Tennis Roger Federer REUTERS/Aly Song
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Uswiss na bingwa nambari moja alipata ushindi wa kishindo katika michuano ya Bercy mwaka jana ambapo alimchua vikali John Isner katika fainali na kumtwanga Juan Martin del Potro katika robo hatua ya fainali huku baadaye katika nusu fainali akimtupilia mbali Rafael Nadal.

Federer anatazamia msimu wa kasi kwa mara nyingine lakini bila ya kujihesabu kama mshindi mara nane wa fainali za world tour zitakazoanza jijini London baada ya kukamilika kwa fainali za Paris.

Pamoja na kukosekana kwa Nadal baada ya kupata majeraha ya goti yaliyomuweka pembeni mwa ulingo Federer atakabiliana na mshindi nambari mbili Novak Djokovic na mshindi wa michuano ya wazi ya Marekani Andy Murray.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.