Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Kocha Roberto Mancini atema cheche dhidi ya makocha wenzake wanaomkosoa

Kocha wa timu ya Manchester City ya nchini Uingereza Roberto Mancini amewataka makocha wenzake kuacha tabia ya kukosoa tabia yake wakati wao pia huwa walalamishi kwa waamuzi. 

Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson akijibizana na kocha wa Manchester City, Roberto Mancini
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson akijibizana na kocha wa Manchester City, Roberto Mancini REUTERS/Nigel Roddis
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo mwenye tambo ameyasema hayo mara baada ya mchezo wa timu yake na klabu ya Aston Villa kuwania kombe la Capital One na kushuhudia timu yake ikikubali kichapo cha mabao 4-2.

Wakati wa mchezo huo Mancini mara kadhaa alionekana akimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo baada ya wachezaji wake kufanyiwa madhambi lakini alishangazwa na hatua ya kocha wa Aston Villa Paul Lambert kumtolea matamshi ya kejeli.

Mancini amesema kuwa alishangazwa na kauli ya kocha huyo ambayo sio ya kiungwana kwakuwa hakutumia ishara yoyote kumkemea mwamuzi wa mchezo huo kuhusu wachezaji wake lakini Lambert akaamua kumvaa kwa maneno.

Akizungumza huku akioneshwa kuchukizwa na matamshi ya kocha mwenzie, Mancini amesema iwapo makocha wa timu nyingine wanataka kumkosoa yeye basi waanze na baadhi ya makocha wa timu kubwa ikiwemo ya Manchester United ambayo kocha wake amekuwa mlalamishi kwa waamuzi.

Kocha huyo mara kadhaa amejikuta akiingia kwenye vita ya maneno na kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, pia kocha wa Everton David Moyes na Mark Hughes wakati alipokuwa kocha wa Fulham.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.