Pata taarifa kuu
UHISPANI-UINGEREZA-URENO-UJERUMANI

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Europa Atletico Madrid waanza mashindano hayo kwa ushindi sawa la Liverpool

Bingwa Mtetezi wa Kombe la Europa Atletico Madrid ameanza vyema harakati zake za kutetea taji lake baada ya kuibuka na ushindi wa ugegeni wa magoli 3-0 mbele ya Hapoel Tel-Avivi.

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia moja ya goli walilofunga kwenye mchezo dhidi ya Young Boys
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia moja ya goli walilofunga kwenye mchezo dhidi ya Young Boys
Matangazo ya kibiashara

Magoli ya Atletico Madrid yamekwamisha kimiani na Cristian Rodriguez, Diego Costa na Raul Garcia huku mchezo mwingine wa Kundi B ukishuhudia Viktoria Plzen ikishinda kwa magoli 3-1 dhidi ya Academica Coimbra.

Kundi A limeshuhudia Vijogoo vya Jiji Liverpool vikiibuka na ushindi wa magoli 5-3 mbele ya Young Boys wakati mchezo mwingine umeshuhudia Udinese ya Italia ikitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Anji Makhatchkala ya urusi.

Borussi Moenchengladbach yenyewe ikaenda sare ya bila kufungana na AEL Limassol wakati vinaja wa Fenerbahce ya Uturuki wakishindwa kupata ushindi wa nyumbani kwenye mchezo wao dhidhi ya Marseille baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 2-2.

Kundi D limeshuhudia vijana wa Bordeaux ya Ufaransa ikipata ushindi mnono wa magoli 4-0 mbele ya Club Bruges ya Ubelgiji huku Newcastle United ya Uingereza ikishinda kuchomoza na ushindi mbele ya Maritimo Funchal ya Ureno kwa kwenda sare ya bila kufungana.

FC Copenhagen ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Molde ya Norway wakati miamba ya Ujerumani VfB Stuttgart wakibanwa mbavu na Steaua Bucharest ya Romania na kwenda sare ya magoli 2-2.

Michezo mingine Dnipropetrovsk ikashinda kwa magoli 2-0 dhidi ya PSV Eindhoven wakati Napoli ya Italia ikichomoza na ushindi mnono wa magoli 4-0 mbele ya AIK Solna huku Genk ikishinda mwa goli 2-0 dhidi ya Video Fehervar.

Inter Milan ikabanwa nyumbani na kuambulia sare ya magoli 2-2 mbele ya Rubin Kazan huku Sporting Lisbon wakimaliza mchezo kwa sare tasa wakiwa wanapambana na FC Basel.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.