Pata taarifa kuu
michezo

Roger Federer amtaka Nadal kushiriki michuano ya kombe la Davis

Bingwa wa tennis kwa upande wa wanaume Roger Federer amemtaka nyota mwenzie Rafael Nadal kurejea ulingoni mwaka huu pamoja na hofu kwamba hasimu wake huyo raia wa Uhispania hatoshiriki nusu fainali za michuano ya kombe la Davis.

Bingwa mara saba katika michuano ya French Open,Rafael Nadal
Bingwa mara saba katika michuano ya French Open,Rafael Nadal REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Nadal,ambaye amekuwa bingwa mara saba katika michuano ya wazi ya Ufaransa hajashiriki mechi tena tangu mshtuko wa mzunguko wa pili katika michuano ya Wimbledon mnamo mwezi June.

Mchezaji huyo alishauriwa kukaa pembeni ya michuano hiyo hadi hali yake kiafya itakapotengemaa jambo ambalo lilichangia akose kushiriki michuano inayoendelea ya wazi ya Marekani ambayo mnamo mwaka 2010 aliibuka bingwa.

Jina la Nadal halijaonekana katika orodha ya timu zilizobainishwa rasmi na mtandao wa kombe la Davis kwa ajili ya michuano ya nusu fainali.

Federer amesema kuwa hajashtushwa na habari hizo bado anamatumaini kuwa nyota mwenzake atakuwa sawa hivi karibuni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.