Pata taarifa kuu
EURO 2012

Uhispania na Italia zatinga hatua ya robo fainali Euro 2012

Michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2012 imeendelea kutimua vumbi hapo jana na kushuhudia vigogo wengine wakitupwa nchi ya michuano hiyo kwenye michezo ya kukamilisha ratiba ya kundi C.

Jesus Navas mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uhispania
Jesus Navas mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uhispania Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mchezo uliopigwa nchini Poland timu ya taifa ya Uhispania ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya Croatia kwenye mchezo ambao umeshuhudia Uhispania wakipata nafasi kwenye dakika za majeruhi.

Goli na dakika za lala salama la mchezaji Jesus Navas lilitosha kuzamisha jahazi la timu ya taufa ya Croatia ambayo wachezaji wake itabidi wajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi ambazo zingeweza kushuhudia timu hiyo ikisonga mbele.

Mara baada ya mchezo huo kocha wa timu ya taifa ya Uhispania Vicente Del Bosque amekiri timu yake kucheza chini ya kiwango na kwamba hata goli lenyewe walilopta lilikuwa ni bahati kwasbabu wachezaji hawakujituma uwanjani.

Kwa upande wake kocha wa timu ya tiafa ya Croatia Slaven Bilic amesema kuwa hana chakuzungumzia lakini aliwapongeza vijana wake kwa mchezo mzuri licha ya kukosa magoli mengi ya wazi.

Kwenye mchezo mwingine timu ya taifa ya Italia ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Ireland kwenye mchezo ambao umeshuhudia Ireland ikiaga mashindano ya mwaka huu hata bila ya alama yoyote kwenye kundi lake baada ya kupata kipigo ha mabao 2-0.

Magoli ya Antonio Cassano na Mario Balotelli yalitosha kuiwezesha timu ya Italia kusonga mebele kwenye hatua ya robo fainali ya michauno ya mwaka huu.

Hii leo kutakuwa na michezo miwili itakayopigwa nchini Ukrain kwa timu taifa ya Sweeden kucheza na Ufaransa huku timu ya taifa ya Uingereza ikicheza na timu ya taifa ya Ukrain.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.