Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Newcastle yakichakaza Chelsea kwenye mbio za kugombea nafasi nne za juu nchini Uingereza

Newcastle United imejiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kugombea nafasi nne za juu katika Ligi Kuu Nchini Uingereza ili iweze kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao baada ya kufanikiwa kuifunga Chelsea ambayo ilikuwa nyumbani Stamford Bridge.

Mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse akishangilia goli lake la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Chelsea
Mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse akishangilia goli lake la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Chelsea
Matangazo ya kibiashara

Magoli mawili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal aliyejiunga na Newcastle mwezi january akitoka Freiburg kwa ada ya £10 milioni Papiss Cisse yalitosha kuwapa ushindi huo wa kwanza nyumbani kwa Chelsea tangu mwaka 1996.

Cisse alifunga katika kila kipindi magoli ya kushangaza ambayo yalimfanya mlindamlango wa Chelsea Petr Cech kutokuwa na uwezo wa kuokomoa michomi iliyopigwa kiufundi na mshambuliaji huyo mahiri.

Magoli haya mawili yanamfanya Cisse afikishe magoli 13 katika michezo yake 12 aliyocheza akiwa amevalia jezi za pundamilia zinazotumiwa na Newcastle tangu ajiunge nao akitokea nchini Ujerumani.

Mchezo huo nusura uingie dosari baada ya Kiungo wa Kimataifa wa Nigeria anayekipiga Chelsea Jon Obi Mikel kumpiga kiwiko kichwani Kiungo wa Newcastle Cheick Toite ambaye alilazimika kuondolewa uwanjani akiwa kwenye machela baada ya kupatiwa matibabu kwa dakika kadhaa.

Kipigo hicho kimsukuma Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo kusema bayana wanakibarua kigumu kuweza kumaliza kwenye nafasi nne za juu licha ya kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich huku jumamosi wakikipiga na Liverpool kwenye fainali ya Kombe la FA.

Kwenye mchezo mwingine ambao uliopigwa jana uliwakutanisha Tottenham dhidi ya Bolton ambao walikuwa nyumbani katika Uwanja wa Reebok ambapo waliambulia kichapo cha magoli 4-1.

Tottenham ambayo inashikilia nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza ilipata magoli yake kupitia Luka Modric kabla Nigel Reo-Coker hajasawazisha ndipo Rafel Van Der Vaart na Emmanuel Adebayo aliyefunga mara mbili hawajaihakikishatimu yao ushindi huo.

Kabla ya mchezo huo kwa mara ya kwanza Kiungo wa Bolton ambaye alipoteza maisha kwa zaidi ya saa moja baada ya kuanguka kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA Fabrice Muamba alionekana hadharani kwa mara ya kwanza na kuzua simanzi kwa mashabiki wa klabu yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.