Pata taarifa kuu
AUSTRALIAN OPEN

Djokovic aweka historia katika mashindano ya Australian Open

Bingwa nambari moja wa mchezo wa Tennesi duniani Novak Djokovic amefanikiwa kuweka historia katika mashindano ya Australian Open baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Bingwa namba moja wa mchezo wa Tennis, Novak Djokovic
Bingwa namba moja wa mchezo wa Tennis, Novak Djokovic Reuters
Matangazo ya kibiashara

Djokovic ambaye alikuwa akipambana na Rafael Nadal alifanikiwa kumshinda mpinzani wake kwa seti 5-7, 6-4, 6-2, 6-7 na 7-5 katika mchezo ambao ulidumu kwa takriban saa tano kuweza kupata mshindi.

Katika mchezo huo Nadal alionekana kumdhibiti vilivyo bingwa huyo na kuonekana kana kwamba angeweza kubadili matokeo lakini haikuwa hivyo kwani katika seti ya pili, Djokovic aliweza kuamka na kurudi kwenye mchezo.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Novak Djokovic hakusita kuonyesha furaha yake pale alipovua shati na kuanza kushangili ambapo wakati akihojiwa kinara huyo alikuwa akitokwa na machozi ya Furaha.

Akizungumzia mchezo wake na Nadal, Djokovic amesema kuwa, haikuwa rahis kwake kuweza kumfunga Nadal kwakuwa alikuwa amejipanga na hakutarajia kupata urahisi.

Djokovic anaungana na wachezaji wengine kama Andre Agassi, Roger Federer na Mats Wilander ambao nao walifanikiwa kuweka historia kwa kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo.

Kwa upande wake Rafael Nadal amempongeza mpinzani na kusema kuwa haikuwa rahisi kwake pia kuweza kumdhibiti bingwa huyo kwa saa tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.