Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAREKANI

Serena Williams kukosa mashindano ya French Open

Mchezaji nambari moja wa zamani wa Tennesi upande wa wanawake Serena Williams amejiondoa kwenye Mashindano ya French Open kutokana na kushindwa kupona baada ya kuwa na maumivu ya mguu kwa muda mrefu.

Serena Williams akiwa ameshinda Taji la Wimbledon Open
Serena Williams akiwa ameshinda Taji la Wimbledon Open Reuters
Matangazo ya kibiashara

Williams ambaye mara ya mwisho alishinda Taji la French Open mwaka 2002 amekuwa akihaha kuyashinda maumivu lakini kwa muda ameshindwa kushiriki mashindano yoyote.

Shirikisho la Tennesi nchini Ufaransa limethibitisha Williams hatoshiriki kwenye Mashindano ya mwaka huu ya French Open ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 22 ya mwezi May.

Williams mwenye umri wa miaka 29 kwa sasa anashika nafasi ya 13 kwa ubora sababu ikiwa ni kutoshiriki kwake kwenye mashindano kutokana na kukabiliwa na maumivu ya mguu.

Mwanadada huyo mahiri kwenye mchezo wa tennesi amesema anamatumaini atarejea tena uwanjani wakati wa majira ya joto na amewashukuru wale wote ambao wameendelea kumuombea apone haraka.

Williams wakati akipambana kushinda maumivu ya mguu mapema mwezi February alikutana na pigo jingine baada ya kuumia misuli ya paja na hivyo kuchangia kumchelewa kurejea uwanjani.

Naye dada yake Serena, Venus ambaye ameshinda mataji saba kati ya hayo yakiwa matano ya Wimbledon naye yupo kwenye mashaka iwapo atashiriki kwenye Mashindano ya French Open.

Venus hajaonekana uwanjani tangu alipoodnolewa kwenye mashindano ya Australian Open mnamo mwezi January akiwa anakabiliwa na maumivu ya paja.

Shirikisho la Tennesi la Ufaransa pia limethibitisha Mchezaji namabri moja wa zamani raia wa Urusi Dinara Safina naye ameondolewa kwenye kinyang'anyiro hicho kutokana na kukabiliwa na maumivu ya mgongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.