Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Manchester City yakata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA

Goli la kujifunga la mshambuliaji wa Kimataifa wa Uingereza anayekipiga katika Klabu ya Tottenham Hotspur Peter Crouch lilitosha kuwapa tiketi Manchester City ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA msimu ujao.

Nembo rasmi ambayo inatumiwa na Klabu ya Manchester City
Nembo rasmi ambayo inatumiwa na Klabu ya Manchester City
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo wa Manchester City umeifanya Klabu hiyo kijihakikishai nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kwani tayari imefikisha pointi 65 ambazo haziwezi kufikiwa na Liverpool ambayo inashika nafasi ya tano.

Goli hilo la kujifunga la Crouch lilikuja katika dakika ya 30 wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira uliopigwa na James Milner lakini ukamshinda na kujaa wavuni.

Crouch anakumbukwa vyema na Manchester City kwa kuwa msimu uliopita ndiye alizima ndoto zao za kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA nafasi ambayo ilitwaliwa na Tottenham iliyofanikiwa kufika hadi hatua ya robo fainali.

Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany amekiri kufurahishwa na klabu yake kukata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA msimu ujao lakini amesema lengo lao ni kumaliza katika nafasi ya tatu.

Baada ya mchezo huo Kocha wa Manchester City Roberto Mancini amesema lengo lake limetimia kwa kuwa alipowasili kuinoa timu hiyo alisema ni lazima aifanikishe kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya EUFA katika kipindi cha misimu miwili.

Mancini akaongeza tambo kwa kusema wanastahili kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA kwa kuwa wamekuwa na kikosi bora kilichowafanya wamalize katika nafasi nne za juu.

Katika hatua nyingine Mancini amewaonya wachezaji wake kuwa makini na mchezo wao wa Fainali ya Kombe la Chama Cha Soka Uingereza FA ambapo watakumbana na Stoke City.

Kocha huyo amewataka wachezaji wao kupambana kwa nguvu zao zote ili waweze kufanikiwa kutwa kombe hilo katika msimu huu kitu ambacho kitakuwa chachu kwao kufanya vizuri msimu ujao.

Kwa upande wake Kocha wa Tottenham Harry Rekdnapp amesikitishwa na wao kupoteza nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya EUFA kwa msimu wa pili lakini kukesaka kwa wachezaji wake wawili muhimu kumechangia hilo.

Redknapp amesema kukosekana kwa Gareth Bale na Rafael Van Der Vaart ni sababu ya wao kupoteza nafasi hiyo adhimu lakini amefurahishwa na jinsi ambavyo timu yake imecheza kwa kipindi chote cha msimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.