Gaza: Mossad ya Israel yasema Hamas imekataa mpango wa kusitisha mapigano
Mossad, idara ya ujasusi ya Israel, imesema leo Jumapili kwamba Hamas ya Palestina imekataa mpango wa hivi karibuni wa kusitisha mapigano uliowekwa mezani wiki moja mapema mjini Cairo na wapatanishi.
Imechapishwa:
Kukataliwa kwa pendekezo lililowasilishwa na nchi tatu zinazopatanisha katika mazungumzo hayo - Marekani, Misri na Qatar - kunaonyesha kuwa kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, Yahya "Sinwarr hataki makubaliano kwa ajili ya misaada ya kibinadamu, wala kurejea kwa mateka," inabaini Mossad (kitengo cha masuala ya kigeni cha idara ya ujasusi ya Israeli), katika taarifa kwa vyombo vya habari katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, saa chache baada ya shambulio la Iran dhidi ya Israel.
Taarifa zaidi zinakujia...