Pata taarifa kuu

Iran yarusha ndege zisizo na rubani na makombora zaidi ya 200 dhidi ya Israel

Iran imezindua mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel Jumamosi Aprili 13 "kutoka katika ardhi yake", ametangaza msemaji wa jeshi la Israel katika hotuba ya televisheni. Walinzi wa Mapinduzi wamethibitisha shambulio hilo, ambalo bado linaendelea kulingana na jeshi la Israeli. Zaidi ya ndege 200 zisizo na rubani na makombora zilirushwa kuelekea Israeli, ambazo "nyingi" zilinaswa.

Vitu vikiruka vikizuiliwa katika anga ya Israeli (hapa, mtazamo kutoka Ashkelon), usiku wa Aprili 13 kuamkiai Aprili 14, 2024, saa chache baada ya Iran kurusha ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel.
Vitu vikiruka vikizuiliwa katika anga ya Israeli (hapa, mtazamo kutoka Ashkelon), usiku wa Aprili 13 kuamkiai Aprili 14, 2024, saa chache baada ya Iran kurusha ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel. REUTERS - Amir Cohen
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

♦ Zaidi ya ndege 200 zisizo na rubani na makombora vilirushwa kuelekea Israel Jumamosi jioni na Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, Hezbollah ya Lebanon na Wahouthi wa Yemen. "Idadi kubwa" ya makombora haya yalinaswa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. Lakini shambulio hilo bado "linaendelea", kulingana na jeshi la Israeli.

♦ Milipuko na ving'ora vya maonyo vilianza kusikika angani juu ya mji wa Jerusalem karibu 4:45 usiku saa za kimataifa, na pia katika maeneo kadhaa ya Israeli. Jeshi la Israel linazungumzia "uharibifu mdogo" katika kambi ya kijeshi na mtu mmoja aliyejeruhiwa, huku shirika la habari la serikali la Iran, IRNA, likizungumzia "uharibifu mkubwa katika kambi muhimu zaidi ya kikosi cha anga huko Negev".

♦ Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu wa Israel ameitisha kikao cha baraza la mawaziri la vita katika katika eneo lisilojulikana chini ya ulinzi mkali. Baada ya mkutano huo alizungumza na Rais wa Marekani Joe Biden.

♦ Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapanga kukutana kwa dharura leo Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.