Pata taarifa kuu

Mlango wa bahari wa Hormuz: Iran yakamata meli ya makontena ya Israel

Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi, jeshi la wasomi wa Iran, lilikamata meli ya biashara ya bilionea wa Israel katika Mlango wa bahari wa Hormuz mnamo Aprili 13.

Picha hii iliyochukuliwa kutoka kwa video ya UGC, iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii mnamo Aprili 13, 2024, inaonyesha Walinzi wa Mapinduzi ya Irani wakishuka kwenye meli ya kontena iitwayo MSC Aries, karibu na Mlango wa Hormuz.
Picha hii iliyochukuliwa kutoka kwa video ya UGC, iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii mnamo Aprili 13, 2024, inaonyesha Walinzi wa Mapinduzi ya Irani wakishuka kwenye meli ya kontena iitwayo MSC Aries, karibu na Mlango wa Hormuz. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni televisheni ya Iran iliyothibitisha habari hii, anaripoti mwandishi wetu wa mjini Tehran, Siavosh Ghazi. Meli hiyo iitwayo 'MCS Aries' inamilikiwa na bilionea wa Israel. Ilikamatwa na Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi la Sepah. Meli hiyo ilielekezwa kwenye maji ya eneo la Irani.

Kwa mujibu wa baadhi ya tovuti zilizobobea, hii ni sehemu ya jibu la Tehran kwa shambulio la ubalozi mdogo wa Aprili 1, ambalo lilisababisha vifo vya watu kumi na sita, wakiwemo maafisa wawili wa ngazi za juu wa kikosi maalumu cha Walinzi wa Mapinduzi. Hii inaonyesha kuwa Tehran iko tayari kwa hali yoyote itakayotokea.

Kwa hakika, matamko yanaongezeka nchini Iran kuhusu jibu dhidi ya Israel. Vyombo vya habari vya Irani vinazungumzia juu ya mashambulio dhidi ya Israeli kwa kutumia makombora ya usahihi na ndege zisizo na rubani.

Katika nakala zilizotumwa kwa vyombo vya habari vya kigeni vilivyoko mjini Tehran, serikali ya Iran imedai kuwa shambulio la Iran baada ya kuharibiwa kwa ubalozi mdogo wa Iran ni hatua halali.

Wakati huo huo, Iran inaonya kwamba ikiwa serikali ya Israel itachukua hatua, kutakuwa na jibu kali zaidi kutoka kwa Iran na matarajio ya mzozo huo kuongezeka katika eneo lote.

Katika siku za hivi karibuni, washirika wa Tehran katika ukanda huo, hususan Hezbollah ya Lebanon, Houthis nchini Yemen na wanamgambo wa Kishia wa Iraq, wameongeza mashambulizi dhidi ya Israel.

Tehran imeionya Washington dhidi ya uwezekano wowote wa kuiunga mkono Israel katika tukio la shambulio la Iran. Kambi za Marekani zinaweza kulengwa na Tehran na washirika wake.

Wafanyakazi 25 wako kwenye meli iliyokamatwa Jumamosi hii, amesema mmiliki wa meli hiyo ya MSC, raia mwenye uraia pacha Italia na Uswisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.