Maofisa wa jeshi la Iran wauuawa katika shambulio la Israeli
Nairobi – Iran imethibitisha kuuawa kwa maofisa wake kadhaa wa jeshi akiwemo kamanda wa juu kwenye jeshi lake, katika shambulio la Israel lililotekelezwa kulenga jengo lililo jirani na ubalozi wake mjini Damascus, Syria.
Imechapishwa:
Cheza - 00:42
Kwa mujibu wa maofisa wa Iran, watu 7 waliuawa katika shambulio hilo ambalo inasema litajibiwa kwa nguvu zote, tangazo linalotishia kuzuka kwa mzozo mwingine kwenye eneo la mashariki ya kati.
Iran imewataja maofisa wake wajuu waliouawa kuwa ni Brigedia Jenerali Mohammed Reza na Brigedia Mohammed Hadi haji, ambao walikuwa wanaongoza vikosi vya kijeshi vinavyofanya operesheni zake Syria, Lebanon na Palestina.
Israel haijasema chochote kuhusiana na shambulio hilo wala kuthibitisha ikiwa lilikuwa mahsusi kuwalenga maofisa hao, tukio ambalo mshirika wake wa karibu Marekani, naye amekuwa kimya ingawa imekiri kufahamu kilichotokea.
Katika hatua nyingine wizara ya mambo ya nje ya Urusi, imetoa taarifa kukashifu shambulio hilo ililosema halikubaliki.