Pata taarifa kuu

Watoto watatu wa kiongozi wa Hamas wauawa na Israel Gaza

Kiongozi wa Hamas anashikilia kuwa vifo vya wanawe watatu katika shambulizi la Israel havitabadili msimamo wa kundi la Hamas katika mazungumzo ya usitishwaji mapigano huko Gaza, ambapo mashambulizi ya anga ya Israel yanaendelea leo Alhamisi baada ya miezi sita ya vita.

Ismaïl Haniyeh ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas mwaka 2017, anaishi kati ya Qatar na Uturuki.
Ismaïl Haniyeh ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas mwaka 2017, anaishi kati ya Qatar na Uturuki. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano Hamas ilitangaza kwamba watoto watatu na wajukuu wanne wa Ismail Haniyeh, kiongozi wa kundi hilo waliuawa katika shambulio la anga katika kambi ya wakimbizi ya Shati huko Gaza (kaskazini), ambapo familia ilikuwa ikiwatembelea jamaa katika siku ya kwanza ya sherehe za Eid al-Fitr kuashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.

"Namshukuru Mungu kwa heshima iliyoletwa kwetu na kuuawa shahidi kwa wanangu watatu na baadhi ya wajukuu zangu," Bw Haniyeh, anayeishi Doha, nchini Qatar, ameiambia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar. "Adui alilenga gari walilokuwamo."

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limewaua katika shambulio la anga watoto watatu wa Bwana Haniyeh, waliotajwa kama "maafisa wa kijeshi wa kundi la kigaidi la Hamas", shambulio ambalo linakuja wakati wapatanishi wa Qatar, Misri na Marekani wakisubiri majibu ya Hamas kwa pendekezo lao kuhusu usitishwaji mapigano na Israeli, linalohusishwa na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza.

"Adui anadhani anaweza kuvunja nia ya watu wetu na kuwasukuma viongozi kufanya makubaliano (...) Anaota! Umwagaji damu huu utatufanya tuwe imara zaidi," ameongeza Bw. Haniyeh. "Madai yetu yako wazi na hatutayaacha iwapo adui anaamini kuwa kuwalenga wanangu katika kilele cha mazungumzo na kabla ya Hamas kutoa majibu yake, kutashinikiza Hamas kubadilisha msimamo wake, amekosea," ameongeza kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh.

Ismaïl Haniyeh ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas mwaka 2017, anaishi kati ya Qatar na Uturuki. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliwasilisha salamu za rambirambi kwake siku ya Jumatano, na Rais wa Iran Ebrahim Raïssi na nambari 2 wa Hezbollah ya Lebanon, Naïm Qassem, waliwasiliana naye pia kumpa rambirambi, Hamas imesema katika taarifa.

- "Shambulio" dhidi ya Israeli -

Iran "inatishia kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Israel", alitangaza mjini Washington Rais wa Marekani Joe Biden muda mfupi baada ya kutangazwa kwa vifo vya watoto wa Ismail Haniyeh, lakini hasa baada ya kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei kusema siku ya Jumatano kwamba Israeli "itaadhibiwa" kwa shambulio baya dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus mnamo Aprili 1.

Ishara ya mvutano katika siku za hivi karibuni, shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa lilitangaza siku ya Jumatano kusitisha safari zake za ndege kwenda na kurudi Tehran, pengine hadi Alhamisi, "kwa sababu ya hali ya sasa ya Mashariki ya Kati".

"Kama nilivyomwambia Waziri Mkuu (Benjamin) Netanyahu, dhamira yetu kwa usalama wa Israeli, licha ya vitisho hivi kutoka kwa Iran na washirika wake, haitetereka," Biden alisema. "Narudia tena: bila kuyumba. Tutafanya kila tuwezalo kulinda usalama wa Israeli," alingeza, akihimiza Hamas, mshirika wa Tehran, "kusonga mbele" juu ya pendekezo la kusitisha mapigano huko Gaza.

Pendekezo la wapatanishi linatoa usitishaji vita wa wiki sita, kuachiliwa kwa mateka 42 wanaoshikiliwa Gaza badala ya Wapalestina 800 hadi 900 wanaozuiliwa na Israel, kuingia kwa lori 400 hadi 500 za misaada kila siku Gaza na wakazi wa kaskazini kurejea nyumbani Gaza, kwa mujibu wa chanzo cha Hamas.

Hamas ilirejelea wiki iliyopita madai yake ya makubaliano yoyote: usitishaji vita wa uhakika, kuondoka kwa Israel kutoka Gaza, ongezeko kubwa la misaada ya kibinadamu, kurejea kwa waliokimbia makazi yao na makubaliano "thabiti" ya kubadilishana mateka na wafungwa wa Kipalestina.

Licha ya wito wa kusitishwa kwa mapigano, mashambulizi ya Israel yameendelea mapema Alhamisi katika Ukanda wa Gaza, hasa kusini mwa eneo hilo, mshahidi wanasema.

Israel iliapa "kuiangamiza" Hamas baada ya shambulio lisilokuwa na kifani lililotekelezwa tarehe 7 Oktoba na makomando wa kundi hilo la wanamgambo wa Kipalestina walioingia kutoka Gaza kusini mwa Israel, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu 1,170, wengi wao wakiwa raia na kupelekea zaidi ya watu 250 kati yao 129 wanasalia kizuizini huko Gaza, pamoja na vifo 34, kulingana na data ya Israeli.

Mashambulizi ya Israel hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 33,482, hasa raia, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Hamas, kundi linalochukuliwa kuwa la "kigaidi" na Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya na lililo madarakani tangu Juni 2007 huko Gaza.

- "Eid ya yasherehekewa katika mazingira magumu" -

Katika eneo lililoharibiwa la Wapalestina, kati ya magofu au katika makazi yao, Wapalestina wengi walisali, karibu na mikate midogo iliyoandaliwa licha ya uhaba, wakati wa sikukuu ya Eid al-Fitr.

Chini ya shinikizo kutoka kwa miji mikuu mingi kuruhusu misaada zaidi katika ardhi ya Palestina, Israel imeongeza lori za misaada ya kibinadamu zinazoingia Gaza.

"Mwezi uliopita wastani wa kila siku ulikuwa lori 213 na kabla ya hapo ulikuwa lori 170," alisema waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant siku ya Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.