Pata taarifa kuu

Lebanon: Hezbollah yarusha 'dazeni' ya roketi kwenye ngome za Israeli

Vita kati ya Lebanon na Israel viliendelea kupamba moto siku ya Ijumaa, Aprili 12, mapema jioni, katikati mwa vitisho vya Irani vya kuishambulia Israeli kujibu shambulio la Aprili 1, dhidi ya ubalozi mdogo wa Irani huko Damascus. Shambulio hili linalohusishwa na Israel uliwaua askari saba wa kikosi cha walinzi wa Mapinduzi ya Iran, wakiwemo majenerali wawili.

Mfumowa ulinzi wa anga wa Israel wanasa roketi zinazorushwa na wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon, Aprili 12, 2024.
Mfumowa ulinzi wa anga wa Israel wanasa roketi zinazorushwa na wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon, Aprili 12, 2024. © AYAL MARGOLIN / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Huenda hili ndio shambulio kubwa zaidi la roketi zilizorushwa na Hezbollah dhidi ya Israel tangu kuanza kwa mapigano kwenye uwanaja wa vita kati ya Lebanon na Israel tarehe 8 Oktoba. Zaidi ya makombora 80 yalirushwa ndani ya dakika chache tu kuelekea Galilaya na Golan ya Syria iliyokaliwa na kushikiliwa na Israel, anaripoti mwandishi wetu wa Beirut, Paul Khalifeh.

Hezbollah imebaini, katika taarifa kwa vyombo vya habari, kwamba ililenga kikosi cha ardhini cha Israel katika shambulio hilo la roketi. Chama cha Hassan Nasrallah pia kilituma ndege zisizo na rubani za Kamikaze siku ya Ijumaa na kushambulia angalau ngome tano za kijeshi au maeneo ya upande mwingine wa mpaka.

Jeshi la Israel limebaini kwa upande wake kwamba "takriban roketi 40 ziligunduliwa zikirushwa kutoka eneo la Lebanon, baadhi yake zilinaswa". "Hakuna majeraha yaliyoripotiwa," jeshi limesema, na kuongeza kuwa hapo awali lilikuwa limenasa "ndege mbili zisizo na rubani zilizojaa vilipuzi za Hezbollah".

Jeshi la Israeli halikukaa kimya baada ya shambulio la roketi la Hezbollah. Kikosi cha wanahewa kilifanya mashambulio kadhaa dhidi ya maeneo manne ya mpaka wa Lebanon, na kikosi cha ardhini kilirusha makombora kadhaa kwenye sehemu nyingi za vita ambazo zinaenea zaidi ya kilomita 120, kutoka Bahari ya Mediterania hadi chini ya Golan. Ndege za Israel pia ziliruka viunga vya kusini mwa Beirut, ngome kuu ya Hezbollah, na eneo la Mlima Lebanon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.