Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza: Wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Marekani wauawa

Wasaidizi wa shirika lisilo la kiserikali la Marekani ambalo hupeleka chakula katika Ukanda wa Gaza unaotishiwa na njaa waliuawa katika shambulio la Israel siku ya Jumatatu Aprili 1, mwanzilishi wake ametangaza, huku Hamas ikiripoti wahanga watano, ikiwa ni pamoja na wageni wanne.

Wapalestina wakiwa wamebeba mwili wa mtu kufuatia shambulio la anga la Israel katika Hospitali ya Al Aqsa huko Deir al Balah, Ukanda wa Gaza, Jumatatu, Aprili 1, 2024. Mamlaka ya matibabu ya Gaza inasema shambulio la anga la Israel liliwaua wafanyakazi wanne wa kimataifa wa kutoa misaada kutoka shirika la kihisani la World Central Kitchen na Dereva raia wa Palestina baada ya kusaidia kupeleka chakula na vifaa vingine kaskazini mwa Gaza, ambavyo viliwasili kwa boti.
Wapalestina wakiwa wamebeba mwili wa mtu kufuatia shambulio la anga la Israel katika Hospitali ya Al Aqsa huko Deir al Balah, Ukanda wa Gaza, Jumatatu, Aprili 1, 2024. Mamlaka ya matibabu ya Gaza inasema shambulio la anga la Israel liliwaua wafanyakazi wanne wa kimataifa wa kutoa misaada kutoka shirika la kihisani la World Central Kitchen na Dereva raia wa Palestina baada ya kusaidia kupeleka chakula na vifaa vingine kaskazini mwa Gaza, ambavyo viliwasili kwa boti. AP - Abdel Kareem Hana
Matangazo ya kibiashara

"Leo, World Central Kitchen imepoteza dada na kaka zake kadhaa katika shambulio a jeshi la Israeli huko Gaza," ametangaza kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) José Andrés, mkuu na mwanzilishi wa shirika hili lenye makao yake nchini Marekani. Waliuawa "wakati wakifanya kazi ya kuunga mkono kazi yetu ya kibinadamu ya kupeleka chakula Gaza," kulingana na taarifa tofauti kutoka kwa shirika hilo, ikilaani kuwa ni "janga."

Marekani, ambayo inazidi kujitenga na mshirika wake Israel baada ya karibu miezi sita ya vita katika Ukanda wa Gaza, imetangaza kuwa "imefadhaishwa sana" na tukio hili. "Tumehuzunishwa na tunasikitishwa sana shambulio hili," msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa Adrienne Watson amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Wafanyakazi wa misaada lazima walindwe wanapotoa misaada inayohitajika, na tunaitaka Israel kuchunguza mara moja kilichotokea," ameongeza.

Miili mitano na pasipoti tatu za kigeni karibu na maiti

Wizara ya Afya ya Hamas imeripoti waathiriwa watano waliofikishwa katika hospitali huko Deir el-Balah, baada ya "shambulio la anga la Israeli lililolenga gari la shirika la Marekani la World Central Kitchen" katikati mwa Ukanda wa Gaza. "Wana uraia wa Uingereza, Australia na Poland na mtu wa nne ni raia wa nchi gani," chanzo hiki cha Hamas kimeripoti katika taarifa nyingine, kikibainisha kuwa mtu wa tano alikuwa dereva na mkalimani, raia wa Palestina.

Mwandishi wa shirka la habari la AFP aliona miili mitano na pasi tatu za kusafiria za kigeni karibu na maiti hizo katika hospitali ya Al Aqsa Martyrs huko Deir el-Balah. Picha za miili hii na pasipoti pia zinazunguka kwenye mitandao ya kijamii.

Jeshi la Israel limesema "linachunguza tukio hilo la kusikitisha kwa kiwango cha juu zaidi ili kuelewa mazingira" na linahakikisha kwamba "lilifanya kazi kwa karibu na WCK" kwa usambazaji wake wa misaada. Shirika la World Central Kitchen linahusika katika kutuma msaada kwa boti kutoka Cyprus hadi Gaza na kujenga gati ya muda katika eneo la Palestina lililozingirwa. Boti ya kwanza ilishusha shehena yake hapo katikati ya mwezi Machi chini ya usimamizi wa jeshi la Israel.

Takriban miezi sita baada ya kuanza kwa mzozo huo, Wizara ya Afya ya Hamas ilitangaza siku ya Jumatatu vifo vya watu wasiopungua 70 katika saa 24 zilizopita, katika mashambulizi "kadhaa" ya Israeli katika Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.