Pata taarifa kuu

Israeli yatakiwa kuhakikisha msaada wa haraka unawafikia wakaazi wa Gaza

Nairobi – Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, inataka Israeli kuhakikisha kuwa msaada wa haraka wa kibinadamu unawafikia wakaazi wa Gaza, ili kuepusha maafa na ukame kutokana na ukosefu wa chakula, maji na dawa.

Israeli imeendelea na mashambulio katika ukanda wa Gaza ikisema inawasaka wapiganaji wa Hamas.
Israeli imeendelea na mashambulio katika ukanda wa Gaza ikisema inawasaka wapiganaji wa Hamas. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Hague,wamesema Wapalestina wapo kwenye hatari kubwa ya kukabiliwa na ukame na kuhatarisha maisha yao.

Hatua hii imekuja baada ya Afrika Kusini kwenda kwenye Mahakama hiyo na kuishtaki Israeli huku wakiitaka kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wakaazi wa Gaza wanaoendelea kuteseka.

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema iwapo hali itaendelea kuwa hivi, watoto wengi hasa Kaskazini mwa Gaza, wapo kwenye hatariya kupoteza maisha kwa sababu ya utapiamlo.

Wakati hayo yakijiri Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa, wanajeshi wa nchi yake wanajiandaa kuanza operesheni ya ardhini kwenye mji wa Rafah.

Israeli imeendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza, licha ya kupitihswa kwa azimio kwenye Umoja wa Mataifa, kutaka vita vinavyoendelea kukomeshwa ili misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapalestina na kuachiwa huru kwa mateka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.