Pata taarifa kuu

UNSC yapitisha azimio la 'kusitisha mapigano mara moja' Gaza

Mjini New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura, leo Jumatatu, Machi 25, kwa kura 14 kuunga mkono rasimi ya azimio la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano huko Gaza. Azimio hili pia linataka kuachiliwa mara moja kwa mateka na linataka madaktari na wafanyakazi wa kibinadamu waweze kuwaona haraka iwezekanavyo. Ilichukua miezi mitano na wiki tatu kwa Baraza kukubaliana na kutaka kusitisha milipuko ya mabomu kwa sauti moja.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Machi 25, 2024.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Machi 25, 2024. AFP - ANGELA WEISS
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Usitishaji huu wa mapigano huko Gaza unaodaiwa rasmi na jumuiya ya kimataifa umepangwa tu kwa muda wa mwezi wa Ramadhani. Hii inaonyesha jinsi mazungumzo yanavyoendelea kuwa na mvutano mjini New York. Bila shaka yanaonyesha jinsi hali ilivyo katika ukanda huo. Wito wa kusitishwa kwa vita kwa muda wa mwezi wa Ramadhani ulipendekezwa na Sudan siku kumi zilizopita, na ingekuwa ishara mbaya sana ikiwa Marekani haingekubali na kuuzuia kwa Gaza.

Katika siku za hivi karibuni, Joe Biden amebadilisha msimamo wake kuelekea mshirika wake  Israeli. Hatimaye alikuwa tayari kudai kusitishwa kwa mapigano, jambo ambalo Washington ilikuwa imezuia kwa zaidi ya miezi mitano. Lakini ukaidi wa Benjamin Netanyahu juu ya uwezekano wa kushambuliwa kwa Rafah unamsukuma kupaza sauti yake na kutomlinda tena bila masharti katika Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, Washington haikubali usitishaji vita wa kudumu. Kwa hakika, azimio hili bado lilitoa, saa chache kabla ya kupiga kura, kwa ajili ya kusitisha mapigano kwa muda wa mwezi wa Ramadhani, na wazo la kufikia makubaliano ya kudumu. Marekani ilijadili muda usio wazi zaidi kwa makubaliano ya kudumu dakika za mwisho, ishara kwamba Washington bado inataka kubaki na njia ya kuweka shinikizo kwa Israeli na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.