Pata taarifa kuu

Norway yaonya kuhusu operesheni ya kijeshi ya Israel katika mji wa Rafah

Mkuu wa Diplomasia ya Norway ameonya leo Jumanne dhidi ya mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Rafah, kimbilio la mwisho la Wapalestina zaidi ya milioni moja katika Ukanda wa Gaza, na kutoa wito wa "kufikiwa makubaliano ya kudumu ya kusitishwa kwa mapigano". 

Wapalestina wazima gari lililokuwa linawaka moto lililopigwa na shambulio la Israeli, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, mnamo Februari 10.
Wapalestina wazima gari lililokuwa linawaka moto lililopigwa na shambulio la Israeli, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, mnamo Februari 10. © Ibraheem Abu Mustafa / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

"Ninasisitiza kwa nguvu onyo langu dhidi ya operesheni ya ardhini huko Rafah. Hakuna maeneo salama tena Gaza,” ameandika Espen Barth Eide kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). "Operesheni ya ardhini itazidisha hali mbaya ambayo tayari ni janga na kufanya msaada wa kibinadamu kuwa ngumu," ameongeza. "Tunahitaji usitishaji mapigano wa kudumu sasa."

Hamas inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzuia mashambulizi dhidi ya Rafah

Baada ya kuachiliwa kwa mateka wawili wa Israel na jeshi, Benjamin Netanyahu alirejelea siku ya Jumatatu azimio lake la kuendeleza "shinikizo la kijeshi hadi ushindi kamili" dhidi ya Hamas, ambayo Rafah ni "ngome ya mwisho, kwa mujibu Bw. Netanyahu." Hamas inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzuia mashambulizi haya. Osama Hamdane, ambaye ni mmoja wa viongozi wa Hamas, ambaye alizungumza jana usiku huko Beirut katika mahojiano na mwandishi wetu maalum nchini Lebanon, Nicolas Falez, alisema operesheni ya kijeshi ya Israel katika mji wa Rafah ni kufanya mauaji ya halaiki.

Vitisho vya Israel dhidi ya Rafah ni sehemu ya mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza na yanaonyesha kuwa Israel haifahamu kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ipo. Hii inathibitisha kwamba ndani kabisa Israeli haitaki amani. Wanataka kuwaua watu wa Palestina na kuwafukuza kutoka katika ardhi yao. Haya yalielezwa na Smotrich, Waziri wa Fedha wa Israel, alipotangaza kwamba Israel ilinusurika kwa kuwafukuza Wapalestina mwaka 1948 na kwamba vivyo hivyo vifanywe Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Israel yadai kuua zaidi ya wapiganaji 40 wa Hamas

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, wanajeshi wa Israel wanaoendesha shughuli zao huko Khan Younes na katikati mwa Gaza wamewaangamiza zaidi ya wapiganaji 40 wa Hamas katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Maghala mawili ya silaha pia yaligunduliwa na kuharibiwa ndani ya nyumba zilizoko eneo la Khan Younes.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.