Pata taarifa kuu

Josep Borrell apendekeza Marekani kuipa silaha chache Israel

Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell amependekeza siku ya Jumatatu kuwa Marekani inapaswa kutoa silaha chache kwa Israel ikiwa inabaini kuwa kuna vifo vingi sana kwa upande wa Palestina. "Ikiwa unafikiri watu wengi wanauawa, labda unapaswa kutoa bunduki chache ili kuzuia watu wengi kuuawa. Je, hilo si jambo la kimantiki? ", amewaambia waandishi wa habari, akirejelea kauli za Rais wa Marekani Joe Biden akiona kuwa jibu la Israel kwa Gaza "limepindukia".

Wapalestina wakiwa kwenye foleni wakisubiri kupokea chakula kutokana na uhaba wa chakula, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 17, 2024.
Wapalestina wakiwa kwenye foleni wakisubiri kupokea chakula kutokana na uhaba wa chakula, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 17, 2024. © Mohammed Salem / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

"Kila mtu huenda Tel Aviv akiomba, tafadhali usifanye hivi, linda raia, usiue watu wengi," amesisitiza mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borrell, katika mkutano uliofuata wa mawaziri wa maendeleo wa Umoja wa Ulaya. Lakini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu "hasikii mtu yeyote," ameongeza. "Watawahamisha" Wapalestina. "Wapi? Mwezini? », ameuliza tena, akimaanisha mashambulizi yaliyotangazwa na Israel kusini mwa Ukanda wa Gaza ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina wamekusanyika.

Palestina yaitaka EU kumuwekea vikwazo Netanyahu na mawaziri wengine wanne

Raia wa Palestina siku ya Jumatatu wametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuchukua vikwazo dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mawaziri wengine wanne kwa uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, chama cha mawakili nchini Ufaransa kinachowawakilisha kimesema.

Ombi rasmi limeelekezwa kwa mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell na Wakili Sarah Sameur, wa chama cha mawakili cha Demain, ambacho kinawakilisha Wapalestina 21 wanaoishi katika maeneo tofauti katika Ukingo wa Magharibi. Kinaomba Umoja wa Ulaya kuweka vikwazo, chini ya utawala wa Haki za Kibinadamu, dhidi ya Benjamin Netanyahu na Mawaziri wa Ulinzi Yoav Gallant, Mambo ya Kimkakati Ron Dermer, Usalama wa Taifa Itamar Ben Gvir, na Fedha Bezalel Smotrich, kwa "kuhusika kwao katika uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu”, inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.