Pata taarifa kuu

Netanyahu: 'Shinikizo la kijeshi linaloendelea litafanya iwezekane kuwaachilia mateka wote'

Israel imetangaza siku ya Jumatatu Februari 12, kwamba imepelekea kuachiliwa kwa mateka wawili huko Rafah, lengo la mwisho la mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza, ambapo chama tawala cha Hamas kimeripoti Wapalestina 52 waliuawa wakati wa operesheni hii ya usiku.

Picha ya mateka wa Israel mwenye asili ya Argentina Louis Har iliyowekwa ukutani Tel Aviv miongoni mwa picha za mateka wengine ambao bado wanashikiliwa na Hamas huko Gaza.
Picha ya mateka wa Israel mwenye asili ya Argentina Louis Har iliyowekwa ukutani Tel Aviv miongoni mwa picha za mateka wengine ambao bado wanashikiliwa na Hamas huko Gaza. AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Israel imetangaza siku ya Jumatatu kwamba imepelekea kuachiliwa kwa mateka wawili huko Rafah, lengo la mwisho la mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza, ambapo chama tawala cha Hamas kmeripoti Wapalestina 52 waliuawa wakati wa operesheni hii ya usiku. Mashambulizi ya usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu haikuwa sehemu ya uzinduzi wa mashambulizi haya, lakini ya operesheni ya kuwapata mateka wawili waliotekwa nyara Oktoba 7 wakati wa shambulio ambalo halijawahi kufanywa na wapiganaji wa Hamas kusini mwa Israeli, ikiwa ni mwanzo wa vita hivi.

■ Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema ameagiza jeshi kuandaa mpango wa kuwahamisha raia kutoka Rafah, ambako anapanga kuanzisha "operesheni kubwa" na kushinda vita vya mwisho vya Hamas. Baada ya Mji wa Gaza, wakati huo Khan Younes, Israel sasa inalenga operesheni ya ardhini katika mji huu unaopakana na Misri, kusini mwa Ukanda wa Gaza, kama sehemu ya mashambulizi yake ya kijeshi dhidi ya Hamas.

■ Rais wa Marekani Joe Biden alimsihi Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu "kuhakikisha usalama" wa wakazi wa Palestina huku mataifa kadhaa yakionya kuhusu "janga la kibinadamu" katika tukio la shambulio dhidi ya jiji hilo lenye wakazi wengi. Katika mahojiano na idhaa ya Marekani ya ABC, Benjamin Netanyahu amethibitisha kwamba jeshi la Israel litahakikisha "njia salama" kabla ya shambulio lililopangwa dhidi ya Rafah.

 

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya Hamas, iliyotolewa siku ya Jumatatu, Februari 12, watu 28,340 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, 2023. Imeripoti jumla ya vifo 164 katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Wahanga wengi ni wanawake, vijana na watoto. Pia watu 67,984 wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.