Pata taarifa kuu

Lebanon: Nabatieh yakumbwa na mashambulizi

Wakati Hamas imeandaa mpango wa kusitisha mapigano kwa miezi minne na nusu, katika hatua tatu,, kulingana na kundi hili, kufikia mwisho wa mzozo na Israeli tangu mwezi wa Oktoba, na wakati huo, kuachiliwa kwa mateka, Benjamin Netanyahu alikataa matarajio haya siku ya Jumatano, na kulitaka jeshi "kujiandaa" kwa mashambulizi huko Rafah. Misri, hata hivyo, ilitangaza kufanyika kwa "duru mpya ya mazungumzo" siku ya Alhamisi, Februari 8, ukiwepo ujumbe wa Hamas.

Moshi unafuka kutoka kijiji cha Kfar Kila, kusini mwa Lebanon, karibu na mpaka na Israel, Alhamisi hii, Februari 8, 2024 baada ya shambulio la anga. Kwa mara ya kwanza tangu 2006, mji wa Nabatieh pia umekumbwa na mashambulizi leo.
Moshi unafuka kutoka kijiji cha Kfar Kila, kusini mwa Lebanon, karibu na mpaka na Israel, Alhamisi hii, Februari 8, 2024 baada ya shambulio la anga. Kwa mara ya kwanza tangu 2006, mji wa Nabatieh pia umekumbwa na mashambulizi leo. AFP - RABIH DAHER
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu

■ Wakati Hamas ilithibitisha Jumanne Februari 6 kwamba iliwasilisha majibu yake kwa wapatanishi wa Misri na Qatar, kuhusu pendekezo la mapatano ambayo ilitolewa kwake, Israeli ilikataa mradi huu. Kulingana na Bw. Netanyahu, "kukubali madai ya udanganyifu" ya Hamas "sio tu kwamba hakutasababisha kuachiliwa kwa mateka, lakini kutasababisha mauaji mengine" kama yale ya Oktoba 7. Anatetea kudumisha shinikizo.

■ Benyamin Netanyahu pia alitekeleza kile ambacho serikali yake imekuwa ikitangaza kwa siku kadhaa: "Tumeviamuru vikosi vya ulinzi vya Israeli kuandaa operesheni huko Rafah na vile vile katika kambi mbili" za wakimbizi. Anaziona kama "ngome za mwisho" za Hamas.

■ Vikosi vya Israel vimezidisha mashambulizi ya mabomu katika vitongoji vya Rafah siku ya Alhamisi, kulingana na wakaazi, na kuua watu wasiopungua 11 wakati wa mashambulizi ya anga kwenye nyumba mbili. Vifaru pia vilishambulia sehemu za mashariki mwa Rafah, na hivyo kuzidisha hofu ya wakaazi kufuatia mashambulizi ya ardhini.

■ Operesheni kama hiyo ya ardhini huko Rafah inazua hofu kubwa, ambayo Umoja wa Mataifa umeeleza, ukionya kwamba inaweza "kuanzisha uhalifu wa kivita". Kwa mujibu wa Katibu Mkuu António Guterres, kuingia kwa jeshi la Israel katika mji huu "kutazidisha hali ambayo tayari ni jinamizi la kibinadamu na matokeo yasiyohesabika ya kikanda".

■ "Duru mpya ya mazungumzo" inaanza siku ya Alhamisi mjini Cairo chini ya usimamizi wa Misri na Qatar, inayolenga kupata "utulivu katika Ukanda wa Gaza" pamoja na kubadilishana wafungwa wa Kipalestina na mateka wa Israel, ametangaza afisa wa Misri. Hamas imesema inatuma wajumbe huko Cairo, wakiongozwa na afisa mkuu kutoka ofisi yake ya kisiasa.

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya ya Hamas, iliyowasilishwa Alhamisi Februari 8, watu 27,840 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7, 2023. Waliokufa ni hasa wanawake, vijana na watoto. Pia watu 67,317 wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.