Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel ladai kusambaratisha kikosi cha Hamas huko Khan Yunis

Jeshi la Israel limesambaratisha brigedi ya Hamas ya Palestina huko Khan Younes, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema siku ya Alhamisi, wakati IDF (jeshi la Israel) likizidisha mashambulizi yake katika mji mkuu kusini mwa Ukanda wa Gaza katika wiki za hivi karibuni. "Tunakamilisha misheni zetu huko Khan Younes. Pia tutafika Rafah na kuondoa vikosi vya kigaidi vinavyotutishia,” amesema kuhusu mji huo ulioko kwenye ncha ya kusini ya eneo la Palestina, kwenye mpaka na Misri.

Mwanajeshi wa Israeli akiwa makini huko Khan Younes, Januari 27, 2024.
Mwanajeshi wa Israeli akiwa makini huko Khan Younes, Januari 27, 2024. © Sam McNeil / AP
Matangazo ya kibiashara

 

Raia wengi wa Palestina wamekimbilia kusini mwa Ukanda wa Gaza na kisha kwenda Rafah huku mashambulizi makubwa yaliyoanzishwa na Israel kulipiza kisasi mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7 yakienea hadi kwenye ukanda mdogo wa pwani, wenye wakazi wengi.

Jeshi la Israel hapo awali lililenga mashambulizi yake ya mabomu na operesheni za ardhini kaskazini mwa eneo la Palestina, ambako takriban watu milioni 2.3 wanaishi. Baada ya kudai kuchukua udhibiti wa eneo hilo, jeshi la Israel limezidisha operesheni zake kusini mwa Gaza, hasa ndani na karibu na Khan Yunis.

Mji wa Rafah, ambako ni kivuko pekee cha mpaka na Ukanda wa Gaza usiodhibitiwa na Israel, umekuwa njia kuu ya kupeleka misaada ya kibinadamu katika eneo hilo tangu kuanza kwa vita, huko karibu miezi minne.

Kiongozi wa Hamas, Ismaïl Haniyeh, anatarajiwa Alhamisi hii, Februari 1 au Ijumaa hii nchini Misri kujadili kuhusu mapatano mapya katika Ukanda wa Gaza ambako mapigano na mashambulizi ya Israel yanaendelea licha ya hali mbaya ya kibinadamu. Kaskazini mwa eneo hilo na Ukingo wa Magharibi, pamoja na Lebanon na Hezbollah, hali pia bado ni ya wasiwasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.