Pata taarifa kuu

Benjamin Netanyahu aweka mipaka katika mazungumzo na Hamas

Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu anasema Israel haitaondoa vikosi vyake katika Ukanda wa Gaza na kuwaachilia maelfu ya wafungwa wa Kipalestina ili kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka, akipinga ripoti za vyombo vya habari juu ya uwezekano wa makubaliano ya amani.

Kiongozi wa serikali ya Israeli Benyamin Netanyahu akiwa na baraza lake la mawaziri huko Tel Aviv mnamo Desemba 24, 2023.
Kiongozi wa serikali ya Israeli Benyamin Netanyahu akiwa na baraza lake la mawaziri huko Tel Aviv mnamo Desemba 24, 2023. AFP - OHAD ZWIGENBERG
Matangazo ya kibiashara

 

"Israel haitaondoka Gaza na kamwe kuwaachilia 'maelfu ya magaidi wa Kipalestina" , amesema Waziri Mkuu wa Israel Bejami Netanyahu.

Katika matamshi yaliyotangazwa na televisheni ya Israel, Bw. Netanyahu ameongeza: “Hatutamaliza vita hivi bila ya kuwa tumefikia malengo yake yote. Hii ina maana ya kuiangamiza Hamas, kuwarudisha mateka wetu wote na kuhakikisha kwamba Gaza haileti tishio tena kwa Israel. "

Wakati huo huo mapigano makali yamezuka Jumanne hii, Januari 30 katika eneo lote la Ukanda wa Gaza, lakini hasa huko Khan Younes, wakati ambapo mkuu wa Umoja wa Mataifa anafanya kazi nyuma ya pazia kujaribu kuwashawishi wafadhili waliokasirishwa kudumisha uungaji mkono wao kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA. Mzozo kuhusu UNRWA "unavuruga umakini" kwa mzozo wa kibinadamu huko Gaza, linasema shirika la Afya Duniani, WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.