Pata taarifa kuu

Nchi kadhaa zasitisha ufadhili wao kwa UNRWA

Hatima ya raia huko Gaza inasalia kuwa kiini cha wasiwasi mkubwa Jumamosi hii, Januari 27, siku moja baada ya uamuzi wa mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa inayoitaka Israel kuzuia kitendo chochote kinachowezekana cha "mauaji ya kimbari" katika ardhi ya Palestina. Wasiwasi huu unaelekezwa kwa Khan Younes, mji mkuu ulioko kusini mwa eneo hilo lililozingirwa ambalo limekuwa uwanja wa mapigano makali kati ya jeshi la Israel na Hamas katika siku za hivi karibuni.

Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumamosi hii Januari 27, 2024.
Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumamosi hii Januari 27, 2024. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Mji wa Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, bado unashambuliwa bila kuchoka. Jeshi la Israel linazingatia kwamba hapa ndipo uongozi wa eneo la Hamas umejificha.

■ Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, mvua kubwa ilinyesha na kusababisha mafuriko kwenye kambi za mahema huko Rafah, na kuongeza huzuni ya waliohamishwa ambao walikanyaga maji ya matope wakijaribu kuokoa baadhi ya mali.

■ Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ilisema Israel lazima izuie kitendo chochote kinachowezekana cha "mauaji ya kimbari" huko Gaza. Afrika Kusini iliwasiliha malalamiko yake ya dharura kwa mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, ikisema kuwa Israel inakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mauaji ya Kimbari. Lakini ikiwa amri zake ni za kisheria, Mahakama haina njia ya kuzitekeleza.

■ UNRWA ilitangaza siku ya Ijumaa kuwa ilijitenga na wafanyakazi "kadhaa" wanaoshutumiwa na Israel kwa kuhusishwa na shambulio la Oktoba 7. Kwa kujibu, Marekani na mataifa mengine kadhaa "yatasimamisha kwa muda" ufadhili wote kwa shirika hili la wa Umoja wa Mataifa katika siku zijazo.

■ Jumuiya ya kimataifa ilielezea wasiwasi wake baada ya shambulio la mabomu dhidi ya makao ya shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na kusababisha vifo vya watu kumi na watatu siku ya Jumatano.

■ Kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas mnamo Januari 27, watu 26,257 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu karibu 65,000 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.