Pata taarifa kuu

Hamas yasubiri kufanya mazungumzo ya 'kusitisha mapigano kamili'

Kundi la wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina linasema liko tayari kufanya mazungumzo juu ya usitishwaji kamili wa mapigano wala sio wa muda mfupi, kama inavyopendekezwa baadhi ya nchi za magharibi. 

Wapalestina wakiwasili Rafah, kusini mwa Gaza, baada ya kukimbia mashambulizi ya ardhini na angani ya Israel huko Khan Younes, Jumatatu hii, Januari 29, 2024.
Wapalestina wakiwasili Rafah, kusini mwa Gaza, baada ya kukimbia mashambulizi ya ardhini na angani ya Israel huko Khan Younes, Jumatatu hii, Januari 29, 2024. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

 

"Tunazungumza juu ya usitishaji kamili wa mapigano na sio usitishaji wa muda mfupi," Taher al-Nounou, afisa mkuu wa Hamas, ameliambia shiriika la habari la AFPresse baada ya mikutano ya Paris kati ya maafisa wa Marekani, Israel, Qatar na Misri. 

Mara baada ya mapigano kusitishwa, afisa huyo ameongeza, "maelezo mengine yote yanaweza kujadiliwa", ikiwa ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka zaidi ya mia moja wa Israel ambao bado wanashikiliwa huko Gaza. Mfumo wa mapatano na kuachiliwa kwa mateka utakabidhiwa Hamas, kulingana na shirika la habari la AFP, likinukuu vyanzo kadhaa.

Msemaji wa serikali ya Israel aita UNRWA "Shirika lililo karibu na Hamas"

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem, msemaji wa serikali ya Israel Eylon Levy amechukua hatua zaidi katika shutuma dhidi ya shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina, akitangaza kulingana na Haaretz kwamba "UNRWA ni shirika lililo na uhusiano wa karibu na Hamas." "Hili ndilo shirika ambalo Hamas hutumia kuchafua habari kutoka kwa vyombo vya habari vya kigeni," ameongeza, akinukuu ujumbe kutoka mtandao wa X mbayo shirika hilo liliandika na kisha kufuta kuhusu Hamas kunyang'anya misaada yake. "Sasa kwa kuwa tunatambua ukubwa wa uozo wa shirika hili, tunaweza kuanza kuwawajibisha, hata kama wana herufi UN kwa jina lao," amekemea Bw. Levy.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.