Pata taarifa kuu

Gaza yakumbwa na mashambulizi makali katikati mwa mvutano mkali na wafadhili

Mashambulio makali ya Israel yanaendelea katika Ukanda wa Gaza Jumatatu hii, Januari 29 na mvutano umesalia katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Hali ya kibinadamu katika eneo la Palestina inazidi kuwa mbaya, na nchi tisa hadi sasa zimesitisha ufadhili wowote katika siku zijazo kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

Khan Younes, Januari 29, 2024.
Khan Younes, Januari 29, 2024. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Mji wa Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, unashambuliwa bila kuchoka. Wasiwasi umetanda katika hospitali, ambazo ziko chini ya shinikizo.

■Wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani huko Jordan, ambapo Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi kujibu siku ya Jumapili kwa kulenga makundi yanayoiunga mkono Iran. Iran inakanusha kuhusika na shambulio hilo.

■ Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba Israel inapaswa kuzuiakitendo chochote kinachowezekana cha "mauaji ya kimbari" huko Gaza.

■ Muda mfupi baadaye, UNRWA ilitangaza kuwa inajitenga na wafanyakazi "kadhaa" walioshutumiwa na Israel kwa kuhusishwa na shambulio la Oktoba 7. Kwa kujibu, Marekani na mataifa mengine kadhaa yalitangaza kusitisha kwa muda ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

■ Kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas mnamo Januari 28, watu 26,422 waliuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 65,000 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.