Pata taarifa kuu

Asilimia 30 ya Ukanda wa Gaza umeharibiwa, kulingana na utafiti wa kituo cha satelaiti cha UN

Mapigano kati ya jeshi la Israel na Hamas bado yanaendelea siku ya jumaa, Februari 2 katika Ukanda wa Gaza licha ya ishara za "kwanza" zinazoonyesha makubaliano mapya na kuachiliwa kwa mateka, baada ya karibu miezi minne ya vita.

Picha ya setilaiti ya Ukanda wa Gaza, Januari 30, 2024.
Picha ya setilaiti ya Ukanda wa Gaza, Januari 30, 2024. © Planet Labs PBC via AP
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kukumbuka:

■ Kiongozi wa Hamas, Ismaïl Haniyeh, anatarajiwa nchini Misri kujadili mpango uliobuniwa wa kusitisha mapigano. Usitishaji wa mapigano uliopendekezwa kwa ajili ya usafirishaji wa misaada ya kibinadamu na ubadilishanaji wa mateka na wafungwa wa Kipalestina utazingatiwa. Hamas ilitoa "uthibitisho chanya wa kwanza", suluhu pia "iliyoidhinishwa" na Israel, imesema Qatar, ambayo ni mmoja wa wapatanishi katika mgogoro huo. Hata hivyo, chanzo kilicho karibu na Hamas kimekanusha hilo, na kuongeza kuwa kauli ya Qatar ilikuwa "ya haraka na ya uwongo".

■ Unicef ​​imebaini siku ya Ijumaa kuwa watoto 17,000 huko Gaza walitenganishwa na familia zao wakati wa vita.

■ Baada ya uamuzi wa Marekani wa kuwawekea vikwazo walowezi wanne wa Israel katika Ukingo wa Magharibi, Canada nayo inazingatia vikwazo dhidi ya walowezi hawa katika Ukingo wa Magharibi kutokana na ghasia.

■ Zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia makazi yao wanahofia shambulio jingine la kijeshi la Israel baada ya waziri wa ulinzi wa Israel kuapa kushambulia Rafah, eneo ambalo liliwahi kutajwa kuwa "eneo salama."

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya ya Hamas, Ijumaa Februari 2, watu 27,131 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 66,287 walijeruhiwa. Katika ripoti mpya ya Februari 1, shirika la habari la AFP lilihesabu watu 1,163 waliojeruhiwa kwa upande wa Israeli wakati wa shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.