Pata taarifa kuu

Israel-Hamas: takriban watu 27,585 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken anaendelea na ziara yake Mashariki ya Kati Jumanne Februari 6 ili kujaribu kulazimisha makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas. Kando ya mazungumzo haya ya kidiplomasia, mashambulizi mabaya yanaendelea huko Gaza. Kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya Hamas, takriban watu 27,585 wameuawa katika eneo hilo tangu kuanza kwa vita, wengi wao wakiwa wanawake, vijana na watoto.

Mwanamke akipika nje, wakati Wapalestina , ambao wamekimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya anga ya Israeli, wakipewa hifadhi katika kambi ya hema huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas, karibu na mpaka na Misri huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 6. 2024.
Mwanamke akipika nje, wakati Wapalestina , ambao wamekimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya anga ya Israeli, wakipewa hifadhi katika kambi ya hema huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas, karibu na mpaka na Misri huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 6. 2024. © Mohammed Salem / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Jumatatu Februari 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitangaza kuundwa kwa kamati yenye jukumu la kutathmini "kutoegemea upande wowote" kwa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) baada ya shutuma dhidi ya wafanyakazi wake kadhaa. Wakati nchi kadhaa wafadhili wakuu zimezuia utumaji wa fedha, Uhispania imetangaza kutuma msaada wa ziada wa euro milioni 3.5 kwa UNRWA.

■ Vita vinapoingia mwezi wa tano siku ya Jumatano, Februari 7, Israel kwa mara nyingine imeshambulia kwa mabomu Khan Younes, kusini mwa eneo hilo, ambako viongozi wa Hamas wanajificha, kulingana na mamlaka ya Israel. Kwa mujibu wa jeshi la Israel, kiongozi wa Hamas huko Gaza kwa sasa "yuko mafichoni".

■ Mashambulizi ya anga pia yamelenga Rafah, kusini zaidi, yakilenga shule ya chekechea, kulingana na Hamas. Zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia makazi yao, wanaotishiwa na uhaba na magonjwa ya milipuko, sasa wamejaa kwenye makazi na kambi za muda.

■ Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara mpya katika eneo hilo yenye lengo la kuhimiza usitishaji vita. Baada ya ziara yake mjini Cairo, ambako alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kwa ajili ya majadiliano juu ya mapatano na juu ya mateka wa Israel mikononi mwa Hamas, mkuu wa diplomasia ya Marekani anatarajiwa hasa nchini Qatar.

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya ya Hamas, Jumanne Februari 6, watu 27,585 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 66,978 wamejeeuhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.