Pata taarifa kuu

Gaza: Matarajio ya mashambulizi katika Rafah ni 'ya kutisha', wasema Umoja wa Mataifa

Matarajio ya mashambulizi "halisi" ya jeshi la Israel huko Rafah, kusini kabisa mwa Ukanda wa Gaza, ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina ni wakimbizi, ni "ya kutisha", amesema Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu.

Wapalestina wanakusanyika kwenye eneo la tukio ambapo nyumba moja imelengwa na shambulio la Israeli, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 12, 2024.
Wapalestina wanakusanyika kwenye eneo la tukio ambapo nyumba moja imelengwa na shambulio la Israeli, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 12, 2024. © Ibraheem Abu Mustafa / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Kutokana na mauaji ambayo yametokea hadi sasa huko Gaza, tunaweza kufikiria kabisa kitakachotokea Rafah," Volker Türk amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wakati huo huo Waziri wa Ufaransa wa Ulaya na Mambo ya Nje Stéphane Séjourné amesema Jumatatu kwamba operesheni yoyote ya kijeshi ya Israel katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza "haitakosa haki."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné anazungumza na wanahabari mjini Jerusalem mnamo Februari 5, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné anazungumza na wanahabari mjini Jerusalem mnamo Februari 5, 2024. © Ammar Awad / Reuters

Nayo Washington inapinga mashambulizi ya 'kiwango kikubwa' cha Israel huko Rafah bila hatua yoyote iliyopangwa kwa raia, wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema.

Marekani bado inapinga operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel huko Rafah bila hatua za kuwalinda raia katika mji huu wa Palestina kwenye mpaka na Misri, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Matthew amesema siku ya Jumatatu.

Washington pia imeiomba Israel uchunguzi wa "haraka" kuhusu kifo "cha kuhuzunisha" cha Hind Rajab, msichana mwenye umri wa miaka sita aliyepatikana amekufa katika Ukanda wa Gaza baada ya saa nyingi za kilio cha kuomba msaada, msemaji amesema siku ya Jumatatu. "Ni taarifa ya kuhuzunisha, na ya kusikitisha kwa mtoto huyu na bila shaka kumekuwa na maelfu ya watoto wengine ambao wamekufa kwa sababu ya mzozo huu."

Mwendesha mashtaka wa ICC "ana wasiwasi mkubwa" na mashambulio ya Rafah

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan, ameelezea wasiwasi wake siku ya Jumatatu kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya jeshi la Israel huko Rafah, katika Ukanda wa Gaza, akionya kwamba yeyote atakayekiuka sheria za kimataifa atachukuliwa hatua. "Nina wasiwasi sana na ripoti za mashambulio ya anga na uwezekano wa mashambulizi ya ardhini ya vikosi vya Israeli huko Rafah," Karim Khan amesema katika taarifa iliyochapishwa kwenye X.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Karim Khan akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters.
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Karim Khan akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters. REUTERS - PIROSCHKA VAN DE WOUW
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.