Pata taarifa kuu

Rais wa Palestina azuru Qatar kujadili usitishaji vita

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amewasili Doha siku ya Jumapili kwa mazungumzo ya kupata usitishaji vita katika ukanda wa Gaza pamoja na kiongozi wa Qatar, ambaye nchi yake imekuwa kiini cha juhudi za upatanishi na kinawapa hifadhi viongozi wa kisiasa wa kundi la wanamgambo wa Hamas.

Wakati mamlaka ya Palestina ikiishutumu Israel kwa kutishia vyama vya wapalestina, mashirika yasiyo ya kiserikali yanaituhumu serikali kwa kufanya vivyo hivyo kudhibiti upinzani. Hapa, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, wakati wa mkutano huko Cairo, Februari 12, 2023.
Wakati mamlaka ya Palestina ikiishutumu Israel kwa kutishia vyama vya wapalestina, mashirika yasiyo ya kiserikali yanaituhumu serikali kwa kufanya vivyo hivyo kudhibiti upinzani. Hapa, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, wakati wa mkutano huko Cairo, Februari 12, 2023. © Amr Nabil / AP
Matangazo ya kibiashara

 

Shirika la habari la WAFA la Palestina limesema Mahmoud Abbas atakutana na Amir Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani siku ya Jumatatu, lakini halikusema iwapo pia atakutana na viongozi wa Hamas, kundi ambalo kwa muda mrefu limekuwa na msuguano na Mahmoud Abbas na kundi lake la Fatah. lililopo Ukingo wa Magharibi.

Balozi wa Palestina nchini Qatar Munir Ghannam ameiambia redio ya Sauti ya Palestina siku ya Jumapili kwamba Mahmoud Abbas na Amir wa Qatar watajadili kuhusu juhudi za kufikia usitishaji vita huko Gaza na Israel na njia za kuongeza amani, kusaidia wakaazi milioni 2.3 wa eneo hilo. "Qatar ina jukumu muhimu katika juhudi za kimataifa na upatanishi kufikia usitishaji mapigano. Hii ndiyo sababu uratibu na Qatar, pamoja na Misri, ni muhimu sana kukomesha uchokozi huu dhidi ya raia tu wetu,” amesema Munir Ghannam.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani kuzuru Israel katikati ya wiki ijayo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock atazuru Israel katikati ya wiki ijayo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema siku ya Jumapili. Wakati wa ziara hiyo, amesema anapanga kutoa wito kwa usitishaji vita wakati Israeli inajiandaa kusonga mbele huko Rafah.

“Watu milioni 1.3 wanatafuta ulinzi dhidi ya mapigano katika nafasi ndogo zaidi. Shambulio la jeshi la Israeli huko Rafah litakuwa janga la kibinadamu," aliandika Annalena Baerbock katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi.

"Israel lazima ijilinde dhidi ya ugaidi wa Hamas, lakini wakati huo huo inatakiwa kupunguza mateso ya raia haraka iwezekanavyo. Ndio maana usitishwaji vita ni muhimu, hasa ili mateka waweze kuachiliwa. Nitajadili njia za kufanikisha hili nchini Israel wiki ijayo,” aliongeza katika ujumbe wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.