Pata taarifa kuu

Shambulizi la Israeli Gaza: Qatar yakubali kushiriki katika mradi wa ujenzi mpya

Wiki moja baada ya mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel huko Gaza, eneo la Palestina kwa mara nyingine linakabiliwa na changamoto ya ujenzibaada ya nyumba nyingi kuharibiwa na mashambulizi ya Israel. Katika mkutano na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Nyumba na Kazi za Umma huko Gaza, Naji Sarhan, amesema zaidi ya nyumba 1,750 zilibomolewa au kuharibiwa. Kulingana na Hamas, Qatar imekubali kujenga upya nyumba hizi.

Mwanamke wa Kipalestina atundika nguo alizookota kutoka chini ya vifusi vya nyumba mnamo Agosti 8, 2022 mbele ya nyumba yake, ambayo iliharibiwa vibaya na mashambulizi ya anga ya Israel wiki iliyopita katika mji wa Gaza, saa chache baada ya makualiano ya kusitishwa kwa mapigano kuanza kutekelezwa.
Mwanamke wa Kipalestina atundika nguo alizookota kutoka chini ya vifusi vya nyumba mnamo Agosti 8, 2022 mbele ya nyumba yake, ambayo iliharibiwa vibaya na mashambulizi ya anga ya Israel wiki iliyopita katika mji wa Gaza, saa chache baada ya makualiano ya kusitishwa kwa mapigano kuanza kutekelezwa. AFP - MAHMUD HAMS
Matangazo ya kibiashara

Qatar itashiriki tena katika juhudi za kujenga upya Ukanda wa Gaza.

Kwa vyovyote vile, kauli hiiilitolewa Ijumaa Agosti 12 na Ismaïl Haniyeh bila kutoa maelezo zaidi. Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas pia alimshukuru Emir wa Qatar. Mpango huu, alisema, "utaongeza rekodi ya heshima ya Kamati ya Qatar ya Ujenzi mpya wa Gaza".

Qatar, iliyo karibu na vuguvugu hili la Kiislamu lililo madarakani katika eneo la Palestina, ni mja wa wafadhili wakuu katika eneo hili. Mnamo mwezi wa Mei 2021, mwishoni mwa mashambulizi ya Israeli huko Gaza kwa siku kumi, Qatar ilieahidi kutoa dola milioni 500.

Doha pia inasambaza misaada ya kifedha ili kuchangia hasa katika uendeshaji wa mtambo pekee wa kuzalisha umeme wa Gaza. Lakini pia kulipa mishahara ya watumishi wa umma na kusaidia familia zenye uhitaji.

Mwaka jana, msaada huu ulizuiwa kwa miezi kadhaa na Israel. Malipo yake hatimaye yaliweza kuanza tena mwezi Septemba mwaka uliyopita baada ya kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kuhamisha fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.