Pata taarifa kuu

Joe Biden: 'Sasa tuko karibu sana' na makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka

Mazungumzo yanaharakishwa Jumanne, Novemba 21, kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka walio mikononi mwa kundi la Hamas kwa kubadilishana na usitishwaji mapigano kwa muda katika Ukanda wa Gaza, ambapo jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake dhidi ya kundi hili la wapiganaji wa Hamas bila ya kupumzika.

Waandamanaji wanadai kuachiliwa kwa mateka wa Hamas, huko Gaza, Novemba 21, 2023.
Waandamanaji wanadai kuachiliwa kwa mateka wa Hamas, huko Gaza, Novemba 21, 2023. AFP - AHMAD GHARABLI
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Siku ya Jumanne Qatar imesema kwamba makubaliano yalikuwa karibu sana kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka, kwa kubadilishana na usitishwaji mapigano kwa muda katika eneo la Palestina. "Tunapiga hatua," amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati siku moja kabla, kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Hamas, Ismaïl Haniyeh aliripoti kuendelea kwa mazungumzo ya kuachiliowa huru mateka hao.

■ Zaidi ya majeruhi mia moja wamehamishwa kutoka hospitali ya Indonesia hadi katika jengo la Nasser huko Khan Younes, Hamas ilitangaza Jumatatu jioni. Siku moja kabla, shambulio la anga liliua wagonjwa wasiopungua kumi na wawili katika hospitali ya Indonesia, iliyoko pembezoni mwa kambi kubwa ya wakimbizi wa Kipalestina ya Jabaliya, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas.

■ Siku ya Jumatatu, watoto 28 kati ya 31 waliozaliwa kabla ya wakati waliohamishwa kutoka hospitali ya al-Chifa ya Gaza waliwasili Misri, Shirika la Afya Dunia (WHO) limetangaza.

■ Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia vifo 14,128 tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, ikiwa ni pamoja na watoto 5,840, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas, madarakani katika eneo la Palestina. Tangu wakati huo, zaidi ya Waisraeli 1,200 wameuawa. Jeshi la Israel limeripoti watu 239 wanaoshikiliwa mateka na kundi la wapiganaji wa Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.