Pata taarifa kuu

Brics: Mkutano usio kuwa wa kawaida wafanyika kujadili hali ya Mashariki ya Kati

Brics (Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini) hawana nia ya kuendelea kukaa kimya kuhusiana na kile kinachotokea katika Ukanda wa Gaza: wameamua kuandaa mkutano wa mtandaoni siku ya Jumanne kujadili mzozo huo. Mkutano wa kilele usio wa kawaida unafanyika chini ya uongozi wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Brics.

(Kutoka kushoto kwenda kulia) Rais wa Brazil Lula, mwenzake wa China Xi Jinping, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, karibu na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, wanashiriki katika mkutano wa kilele wa BRICS wa 2023 huko Johannesburg, Agosti. 2023.
(Kutoka kushoto kwenda kulia) Rais wa Brazil Lula, mwenzake wa China Xi Jinping, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, karibu na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, wanashiriki katika mkutano wa kilele wa BRICS wa 2023 huko Johannesburg, Agosti. 2023. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Pamoja kushutumu sheria inayodaiwa ya kimataifa ambayo viongozi hao wanaona inaongozwa na Magharibi. Nchi tano za Brics zitajadili pamoja katika mkutano huu wa mtandaoni kuhusu mzozo unaoendelea: vita vinavyoleta mgawanyiko kati ya nchi za Kusini na Magharibi, nchi hizo zikikosolewa kwa misimamo yao inayochukuliwa kuwa nzuri zaidi kwa Israeli. Kwa hivyo China na Urusi zinaweza kutumaini kuchukua fursa ya shutuma zote kutoka kwa mpinzani wao mkuu Marekani na washirika wake.

Afrika Kusini taongoza mkutano huu wa mtandaoni, huku nchi sita ambazo zinatarajia kujiunga na kundi hilo Januari 1 pia zimealikwa, ambazo ni Argentina, Saudi Arabia, Misri, Ethiopia, Iran na Umoja wa Falme za Kiarabu, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Kundi la watu tofauti sana, ambalo linatumaini kupata msimamo wa pamoja, licha ya maoni tofauti, anaripoti mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès.

Misimamo tofauti kuhusu mzozo wa Gaza

Kwa sababu nchi tano wanachama wa Brics zina tofauti zao: China inataka kujionyesha kama mpatanishi anayewezekana, na Urusi, ambayo Kremlin imethibitisha ushiriki wa Vladimir Putin katika mkutano huu, inatumia vita hivi kushambulia Marekani.

India ya Narendra Modi, kwa upande wake, imejenga uhusiano wa karibu na Israel, na hivi majuzi tu ililaani hasara za raia huko Gaza. India na Ethiopia pia zilijiepusha na kura ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mapatano ya kibinadamu.

Afrika Kusini inaikosoa Israel

Badala yake, Afrika Kusini inaongeza misimamo yake muhimu dhidi ya Israel, ikiomba kufunguliwa kwa uchunguzi na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Serikali ya Afrika Kusini, imekuwa ikizungumza tangu kuanza kwa vita katika kushutumu kile inachoelezea kama "ukatili" unaofanywa katika Ukanda wa Gaza, huku chama tawala cha ANCkikiendelea kuiunga mkono Palestina kila mara.

Pretoria pia iliwrejesha nyumbani wanadiplomasia wake walioko Tel Aviv, wakati Jumatatu hii, Israel pia ilimrejesha nyumbani balozi wake aliyeko Pretoria, kwa "mashauriano". ANC inaunga mkono kufungwa kwa ubalozi wa Israel mjini Pretoria. Nchi hiyo pia ni miongoni mwa mataifa ambayo yamewasilisha ombi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ili kushughulikia kesi ya Gaza, ikitarajia kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel.

  Inabakia kuonekana, kwa hiyo, nini itakuwa maudhui ya tamko la pamoja ambalo linapaswa kupitishwa mwishoni mwa mkutano huu. Nchi tano za Brics (kabla ya upanuzi) kwa vyovyote vile zitakuwa na fursa ya kukutana siku inayofuata, katika mkutano mdogo, kwa kuwa zitashiriki katika mkutano wa kilele wa G20 uliopangwa kufanyika Jumatano hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.