Pata taarifa kuu

Waasi wa Houthi wameteka meli inayomilikwa na mfanyibiashara wa Israeli

Nairobi – Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen, wamedai kuteka meli inayomilikwa na mfanyibiashara raia wa Israeli katika bahari ya Red Sea na wameipeleka pwani ya Yemen.

Mataifa ya Israel, Marekani na Japan yamelaani hatua ya wapiganaji hao kuteka meli hiyo
Mataifa ya Israel, Marekani na Japan yamelaani hatua ya wapiganaji hao kuteka meli hiyo via REUTERS - Owen Foley
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limekuja siku chache baada ya wapiganaji hao kutishia kulenga mali zinazomilikiwa na Israeli katika bahari hiyo kutokana na vita vya na wapiganaji wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa Huthi Yahya Saree kupitia ukurasa wake wa X, zamani ukijulikana kama Twitter amethibitisha kutokea kwa kitendo hicho cha utekaji wa chombo hicho.

Mataifa ya Israel, Marekani na Japan yamelaani hatua ya wapiganaji hao kuteka meli hiyo.

Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, chombo hicho kilikuwa kinamilikiwa na kampuni ya Uingereza na shughuli zake zilikuwa zinaendelezwa na kampuni ya nchini Japan.

Benyamin Netanyahu, Waziri mkuu wa Israeli ameahidi kumaliza kundi la Hamas
Benyamin Netanyahu, Waziri mkuu wa Israeli ameahidi kumaliza kundi la Hamas © Abir Sultan / AP

Aidha msemaji huyo wa Huthi ameeleza kuwa kundi hilo litaendelea kutekeleza “oparesheni za kijeshi dhidi ya kile amesema ni adui wa Israel hadi uchokozi dhidi ya Gaza utakapokoma na uhalifu mbaya dhidi ya ndugu zetu wa Kipalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi ukome.”

Israel imeahidi kumaliza kundi la Hamas ambalo linaoongoza Ukanda wa Gaza, hatua iliyojiri baada ya wapiganaji hao wa Palestina kuwauawa karibia raia 1,200 na kuwateka wengine karibia 240 tarehe saba ya mwezi Oktoba kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka ya Israeli.

Israeli imeendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza
Israeli imeendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza REUTERS - STRINGER

Katika upande mwengine, serikali ya Gaza imesema kuwa raia wake elfu 13 wameuwa katika mashambulio ya wanajeshi wa Israeli katika Ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.