Pata taarifa kuu

Mapigano makali yapamba moto karibu na hospitali ya Indonesia kaskazini mwa Gaza

Vifaru vya Israel vimewekwa karibu na hospitali ya Indonesia kaskazini mwa Gaza ambapo Wapalestina kumi na wawili wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, wizara ya afya ya Hamas imesema Jumatatu.

Sur cette photo fournie par les forces de défense israéliennes, des soldats en opération dans la bande de Gaza, le 20 novembre 2023.
Sur cette photo fournie par les forces de défense israéliennes, des soldats en opération dans la bande de Gaza, le 20 novembre 2023. via REUTERS - ISRAEL DEFENSE FORCES
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israel halikuthibitisha mara moja taarifa kutoka hospitali ya Indonesia, lakini shirika la habari la Palestina WAFA limesema hospitali hiyo kilishambuliwa na vifaru vya Israel.

Sawa na vituo vingine vingi vya afya katika Ukanda wa Gaza, hospitali ya Indonesia, iliyoanzishwa mwaka wa 2016 kwa ufadhili wa mashirika ya Kiindonesia, imesitisha kufanya kazi. Lakini msemaji wa Wizara ya Afya Ashraf Al-Qidreh amesema kuna karibu watu 700, pamoja na timu za matibabu na waliojeruhiwa, ndani ya kituo hicho.

WHO yatayarisha uhamisho wa wagonjwa 291 wa mwisho kutoka Al-Shifa

Shirika la Afya Duniani (WHO) linatayarisha uhamisho wa wagonjwa 291 waliosalia, ambao hawawezi kuhama bila msaada wa matibabu, hadi hospitali zingine huko Gaza.

Zaidi ya watoto 30 wanaozaliwa kabla ya wakati wao walihamishwa siku ya Jumapili kutoka hospitali ya Al-Shifa kwennda Rafah, ili kupata "huduma ya haraka katika chumba cha wagonjwa mahututi watoto wachanga," amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa, Tedros Adhanom Ghebreyesus. "Watoto hawa waliteseka sana" na walipata "athari kubwa," mkurugenzi mkuu wa hospitali katika Ukanda wa Gaza, Mohammed Zaqout, ameviambia vyombo vya habari, akibainisha kuwa watoto wanane walifariki kwa kukosa matunzo kabla ya uhamisho wao, ikiwa ni pamoja na wawili Jumapili asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.