Pata taarifa kuu

WHO inasema imewahamisha watoto njiti zaidi ya 30 kutoka Gaza

Nairobi – Shirika la afya duniani, WHO, limesema limefanikiwa kuwahamisha watoto njiti zaidi ya 30 kutoka katika hospitali kubwa zaidi kwenye eneo la Gaza, shirika hilo likisema linapanga kuwandoa wafanyakazi wa hospitali hiyo katika kile imesema eneo la ukanda wa vifo.

Watoto hao njiti wanahamishwa nchini Misri
Watoto hao njiti wanahamishwa nchini Misri © MOHAMMED ABED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya WHO imekuja saa chache tangu ujumbe wake utembelee hospitali ya Al Shifa, ambayo juma lililopita ilivamiwa na wanajeshi wa Israel.

Aidha rais wa kamisheni ya umoja wa Ulaya, Ursula von de Leyen, amesema suluhu ya kisiasa ndio njia pekee ya kuleta amani kati ya Israel na Palestina.

‘‘Hata wakati tunapowazia leo lazima pia tufikirie siku zijazo zitakuwa aje na namna raia wa Israeli na Palestina wanaweza kuwa na matumaini tena.’’ alisema Ursula von de Leyen.

00:21

Ursula von de Leyen kuhusu Palestina

Haya yanajiri wakati huu Israel ikitoa picha za CCTV ilizosema zinaonesha mateka wakipelekwa kwenye hospitali hiyo na wapiganaji wa Hamas.

Katika upande mwengine, China imesema iko tayari kusaidia katika urejeshaji wa amani katika eneo la Mashariki ya kati.

Wakati wa kikao na waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Beijing Wang Yi, wajumbe kutoka nchi za Kiarabu wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea.  

Ursula von de Leyen, amesema suluhu ya kisiasa ndio njia pekee ya kuleta amani kati ya Israel na Palestina
Ursula von de Leyen, amesema suluhu ya kisiasa ndio njia pekee ya kuleta amani kati ya Israel na Palestina AP - Jean-Francois Badias

Karibia raia elfu 13 wa Palestina wameuawa katika mapigano hayo wakati wengine elfu 30 wakiripotiwa kujeruhiwa kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza.

Nayo Ufransa imesema itatuma meli yake ya kivita iliyobeba msaada ya kimatibabu katika Ukanda wa Gaza, rais Emmanuel Macron amethibitisha hapo jana Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.