Pata taarifa kuu

Gaza: Jibu 'chanya' kutoka kwa Hamas kwa makubaliano juu ya mateka, kulingana na Qatar

Wakati maafisa wa Israel wakisisitiza nia yao ya kupanua soperesheni zao za kijeshi huko Rafah, Umoja wa Mataifa umeonya siku ya Jumanne Februari 6 kwamba "uvamizi wa ardhini" unaofanywa na Israel unaweza "kuwa uhalifu wa kivita", na kusababisha "vifo vingi zaidi", kutokana na msongamano wa watu wa sasa katika jiji. Waziri Mkuu wa Qatar amehakikishia siku ya Jumanne kwamba jibu la Hamas kwa mfumo uliopendekezwa ni "chanya".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, akiwa na Amiri wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, kwenye kasri la Lusail huko Doha, Qatar, Jumanne, Februari 6, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, akiwa na Amiri wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, kwenye kasri la Lusail huko Doha, Qatar, Jumanne, Februari 6, 2024. AP - Mark Schiefelbein
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitangaza Jumatatu Februari 5 kuundwa kwa kamati yenye jukumu la kutathmini "kutoegemea upande wowote" kwa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), baada ya shutuma zinazowalenga wafanyakazi wake kadhaa. Wakati nchi kadhaa wafadhili wakuu zimezuia utumaji wa fedha, Uhispania imetangaza kutuma msaada wa ziada wa euro milioni 3.5 kwa UNRWA.

■ Wakati mamlaka ya Israel ikithibitisha tena nia yake ya kupanua operesheni huko Rafah, kusini mwa Gaza, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba uvamizi wa ardhini unaweza "kuwa uhalifu wa kivita". Katika mpaka na Misri, mji huo sasa ni makazi ya nusu ya wakazi wa Palestina, ambao walikimbilia kutokana na milipuko ya mabomu, hasa kufuatia maelekezo ya Israel. Operesheni kama hiyo huenda ikasababisha "vifo vingi zaidi  vya raia", jiji hilo "lina watu wengi", msemaji wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Jens Laerke ameonya siku ya Jumanne.

■ Vita vinapoingia mwezi wa tano siku ya Jumatano, Februari 7, Israel kwa mara nyingine ilishambulia kwa mabomu Khan Younes, kusini mwa eneo hilo, ambapo kwa mujibu wake viongozi wa Hamas wanajificha. Kwa mujibu wa jeshi la Israel, kiongozi wa Hamas huko Gaza kwa sasa "anakimbia" na kusalia mafichoni".

■ Mashambulizi ya anga pia yamelenga Rafah, yakipiga shule ya chekechea, kulingana na Hamas. Zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia makazi yao, wanaotishiwa na uhaba na magonjwa ya milipuko, sasa wamejaa kwenye makazi na kambi za muda.

■ Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara mpya katika eneo hilo yenye lengo la kuhimiza usitishaji vita. Baada ya ziara yake mjini Cairo, ambako alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kwa ajili ya majadiliano juu ya mapatano na juu ya mateka wa Israel mikononi mwa Hamas, mkuu wa diplomasia ya Marekani anatarajiwa hasa nchini Qatar.

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya ya Hamas, Jumanne Februari 6, watu 27,585 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 66,978 wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.