Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Iran: wanaume wanne wanyongwa, wakituhumiwa kufanya ujasusi wa Israel

Wanaume wanne wamenyongwa leo Jumatatu, Januari 29 alfajiri nchini Iran baada ya kuhukumiwa kifo kwa kushirikiana na idara za kijasusi za Israel katika mpango wa kuhujumu eneo la ulinzi la Iran, shirika la habari la mahakama limetangaza.

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi mjini Tehran tarehe 20 Juni 2023.
Rais wa Iran Ebrahim Raïssi mjini Tehran tarehe 20 Juni 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Wafungwa hao wanne walikamatwa Julai 23, 2022 walipokuwa wakitayarisha operesheni dhidi ya kituo cha Wizara ya Ulinzi huko Isfahan, jiji kubwa katikati mwa Iran, kwa niaba ya Mossad, limesema Mizan Online shirika la habari la mahakama.

Wizara ya Ujasusi wakati huo ilitangaza kwamba "imetambua mtandao wa mafisa wa idara ya kijasusi la Kizayuni, ambayo maafisa wake wote walikamatwa," kwa mujibu wa Mizan. Walihukumiwa kifo mwezi Septemba 2023.

"Waliajiriwa na Mossad"

Kulingana na shirika la habari la mahakama, watu hawa wanne waliajiriwa na Mossad, idara ya ujasusi ya Israeli, "karibu mwaka mmoja na nusu kabla ya operesheni hiyo". Kisha walitumwa kwa nchi za Kiafrika kwa "kozi za mafunzo katika vituo vya kijeshi vya nchi hizi". Maafisa wa Mossad walikuwepo kwenye mafunzo haya, shirika hilo limesema.

Nchi hizo mbili zimekuwa zikihusika katika vita vya siri kwa miaka mingi. Israel inaishutumu Iran, ambayo inakanusha, kwa kutaka kupata bomu la atomiki na inasema inatafuta kwa kila njia kuzuia hilo. Israel pia inataka kukabiliana na ushawishi wa Iran katika Mashariki ya Kati.

Tehran kwa upande wake inaituhumu Israel kuwa nyuma ya mfululizo wa hujuma na mauaji ikilenga mpango wake wa nyuklia.

Mnamo Agosti 2023, Iran ilidai kuvuruga mradi "mgumu zaidi" ulioanzishwa na Mossad "kuharibu" tasnia yake ya makombora ya balistiki. Miezi michache mapema, mwezi Februari, Tehran iliishutumu Israel kwa kuhusika na shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye eneo la kijeshi huko Isfahan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.