Pata taarifa kuu

Iran yailaumu Marekani kwa milipuko iliyosababisha vifo vya watu 95

Nairobi – Iran imeilamu Israeli na Marekani baada ya kutokea kwa milipuko miwili ya bomu iliyosababisha vifo vya watu 95 Kusini mwa nchi hiyo wakati wa kumbukumbu ya aliyekuwa Jenerali wa kikosi cha ukombozi Qasem Soleimani, aliyeuawa baada ya kushambuliwa na jeshi la Marekani miaka minne iliyopita.

ya Mambo ya nje Matthew Miller, imekanusha madai ya kuhusika na mashambulio hayo pamoja na mshirika wake Israeli.
ya Mambo ya nje Matthew Miller, imekanusha madai ya kuhusika na mashambulio hayo pamoja na mshirika wake Israeli. AP - Hadi Mizban
Matangazo ya kibiashara

Mohammad Jamshidi, naibu mshauri wa masuala ya kisiasa kwa rais wa Iran, ametaja mashambulio hayo kama matukio ya kigaidi.

Hata hivyo, Marekani  kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Matthew Miller, imekanusha madai ya kuhusika na mashambulio hayo pamoja na mshirika wake Israeli.

Katibu mkuu wa UN amelaani mashambulio hayo
Katibu mkuu wa UN amelaani mashambulio hayo via REUTERS - WANA NEWS AGENCY

Naye kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, amewalaumu maadui wa nchi yake kwa kutekeleza mashambulizi hayo, na kuapa kulipiza kisasi.

Rais Ebrahim Raisi, ameahirisha ziara yake nchini Uturuki hivi leo, kuomboleza vifo vya raia wake.Alhamisi ni siku ya kitaifa ya maombolezo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, nao pia wamelaani mashambulio hayo.

Mashambulio hayo mawili yalitokea, karibu na msikiti wa Saheb al-Zaman mjini  Kerman, wakati kundi kubwa la watu walipokuwa wamekutana kumkumbuka Jenerali Soleimani aliyeuawa mwaka 2020 jijini Baghdad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.