Pata taarifa kuu

Benyamin Netanyahu ataja 'moja ya siku ngumu zaidi tangu kuanza kwa vita'

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa taarifa kwenye mtandao wa X baada ya tangazo la vifo vya askari wa akiba zaidi ya ishirini waliouawa wakati wa kuporomoka kwa jengo walilokuwemo baada ya kupigwa roketi. Ameeleza mshikamano wake na kuashiria kuwa uchunguzi umefunguliwa kuhusu mazingira ya mkasa huo.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema "ninaomboleza vifo vya askari wetu mashujaa waliouawa kusini mwa Ukanda aw Gaza.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema "ninaomboleza vifo vya askari wetu mashujaa waliouawa kusini mwa Ukanda aw Gaza. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

 

"Jana tulipitia moja ya siku ngumu zaidi tangu kuanza kwa vita," amesema Waziri Mkuu wa Israeli. Nawatakia ujasiri familia za wapiganaji wetu mashujaa waliofariki kwenye uwanja wa vita. Ninajua kwamba kwa familia hizi, maisha yao yanabadilika milele. Ninaomboleza vifo vya askari wetu mashujaa waliouawa. Ninakumbatia familia katika wakati huu mgumu wa huzuni, wa maombolezo na sote tunawaombea afya majeruhi wetu. Jeshi la Israel limefungua uchunguzi kuhusu vifo hivyo. Lazima tujifunze masomo muhimu na kufanya kila kitu katika uwezo wetu kuhifadhi maisha ya wapiganaji wetu. Kwa jina la mashujaa wetu, kwa ajili ya maisha yetu, hatutaacha kupigana hadi ushindi kamili.  "

Wanasiasa wa Israel wanaelezea hisia zao baada ya vifo vya askari 21 wa akiba

Baada ya tangazo la vifo vya askari wa akiba 21 waliouawa Jumatatu katika Ukanda wa Gaza, hisia za viongozi wa kisiasa zinaongezeka nchini Israel kwenye mitandao ya kijamii.

Rais wa Israel Isaac Herzog anazungumza kwenye mtandao wa X kuhusu "asubuhi ngumu isiyoweza kuvumilika". "Nyuma ya kila jina kuna familia ambayo imepoteza," ameongeza. Familia ambayo tunaikumbatia kwa huzuni na uchungu, na wakati huo huo kwa fahari kwa ushujaa wa kizazi, kwa kazi walioifanya na urafiki, kwa kujitolea kwa kazi na kwa upendo wa watu na nchi. [...], ameandika. Hata katika asubuhi hii ya huzuni na ngumu, tuna nguvu na tukumbuke kwamba pamoja tutashinda. "

“Hii ni asubuhi ngumu kwa watu wote wa Israeli, kwa habari ya mkasa mbaya uliotokea jana katika kusini mwa Ukanda wa Gaza. Ningependa kutuma rambirambi zangu za dhati kwa familia za walioangamia na kuwatakia majeruhi ahueni, amesema Waziri Benny Gantz. 

"Asubuhi isiyoweza kuvumilika na habari za uchungu za kuuawa kwa askari wa akiba 21 wa IDF, mashujaa wa Israeli, wapenzi wa ardhi yao na watetezi waliouawa katika Ukanda wa Gaza. Taifa zima la Israeli liko pamoja na nyiniy katika nyakati hizi ngumu. Na Mungu aweke roho zao pema peponi,” amesema kiongozi wa upinzani nchini Israel Yair Lapid.

“Tunainamisha vichwa vyetu na kuwasalimu wapiganaji wetu mashujaa waliojitolea maisha yao kutetea nchi. Rambirambi zangu kwa familia za wanajeshi walioaga dunia na ahueni ya haraka kwa waliojeruhiwa,” amesema Waziri wa zamani wa Ulinzi na kiongozi wa chama cha upinzani cha Yisrael Beytenu Avigdor Liberman.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.