Pata taarifa kuu

Israel: Familia za mateka zavamia Bunge la Israeli

Watu zaidi ya ishirini wamevamia Knesset (Bunge la Israel) mjini Jerusalem Jumatatu hii, Januari 22, kutaka watu wa familia zao, wanaoshikiliwa mateka na Hamas tangu mashambulizi ya Oktoba 7, waachiliwe. Kikao cha Bunge kilisitishwa kwa muda kutokana na hali hiyo.

Moja ya vikao vya Knesset c Baraza la Bunge la Israel), Juni 30, 2022, huko Jerusalem.
Moja ya vikao vya Knesset c Baraza la Bunge la Israel), Juni 30, 2022, huko Jerusalem. © MENAHEM KAHANA/AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Siku moja baada ya maandamano mbele ya makazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, hasira inaendelea nchini Israel. Familia za mateka zilizokasirishwa zinaendelea kudai kuachiliwa mara moja kwa wapendwa wao, hasa kutoka kwa wabunge Jumatatu hii katika Knesset.

"Hamtaketi hapa wakati wanakufa huko"

Muda mfupi baada ya familia hizo kufika Bungeni, mwanamke alishikilia picha za watu watatu wa familia yake ambao walikuwa miongoni mwa watu 253 waliotekwa katika shambulio la mpakani la Hamas Oktoba 7, na kusababisha vita na Israel, kama shirika la habari la Reuters lilivyoripoti.

Kisha mwandamanaji huyo akapaaza sauti akisema: “Ningependa kupata angalau mmoja aliye hai, mmoja kati ya watatu!”

Waandamanaji wengine walishikilia mabango yaliyosomeka: "Hamtaketi hapa wakati wanakufa huko", wakipiga kelele wakisema "Waachilieni sasa hivi, sasa hivi, sasa hivi!", wamedai.

Takriban mateka 130 wanaendelea kushikiliwa huko Gaza, baada ya wengine kurejeshwa nyumbani chini ya mapatano mwezi Novemba na wengine kutangazwa kufariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.