Pata taarifa kuu

Arobaini waangamia katika mashambulizi ya anga karibu na shule Khan Younes

Shirika la Hilali Nyekundu na vyanzo vingine vya hospitali katika Ukanda wa Gaza vinaripoti kuwa takriban watu 40 wameuawa katika shambulio la kijeshi la Israel magharibi mwa Khan Yunis.

Katika hospitali ya Nasser, huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 22, 2024.
Katika hospitali ya Nasser, huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 22, 2024. REUTERS - AHMED ZAKOT
Matangazo ya kibiashara

 

Jeshi la Israel limeripotiwa kushambulia karibu na shule ambapo watu waliokimbia makazi yao wanahifadhiwa, na kurushiana risasi katika eneo hilo kuliendelea. Shirika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa haikuweza kuwasiliana na timu zake za matibabu katika jiji lote na kwamba lilikuwa na ugumu wa kufikia maeneo yaliyoathiriwa.

EU lazima ifanyie kazi suluhisho la serikali mbili nchini Israeli: Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani

Suluhu la mataifa mawili linalowezesha kuishi pamoja kwa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina ndilo "suluhisho pekee" la mzozo uliopo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema leo Jumatatu kabla ya kuelekea kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya. "Wale wote wanaosema hawataki kusikia kuhusu suluhu kama hilo hawajatoa njia mbadala," ameongeza, huku akitoa wito wa "kusitishwa kwa mapigano kwa dharura kwa ajili ya misaada ya kibinadamu" katika vita vinavyopamba moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.