Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza: Mji wa Khan Younes wakumbwa na mashambulizi mabaya

Jeshi la Israel bado linamshambulia kwa mabomu Khan Younes, kitovu cha mapigano kusini mwa Gaza, leo, Januari 22, huku familia za mateka nchini Israel zikiitaka serikali ya Netanyahu kukubali makubaliano na Hamas ili waweze kuachiliwa. Wakati huo huo Mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell anasema hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza "haiwezi kuwa mbaya zaidi".

Khan Younes inakabiliwa na mashambulizi mabaya ya anga, picha iliyopigwa kutoka Rafah, Januari 22, 2024.
Khan Younes inakabiliwa na mashambulizi mabaya ya anga, picha iliyopigwa kutoka Rafah, Januari 22, 2024. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Israel inaendelea na mashambulizi makali zaidi kusini mwa Ukanda wa Gaza. Mji wa Khan Younes unakabiliwa na mashambulizi ya anga na idadi ya vifo imeongezeka. Israeli pia inaendelea kufanya operesheni katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na hali ni mbaya kwenye mpaka na Lebanon.

■ Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu alithibitisha tena siku ya Jumapili upinzani wake kwa "uhuru wa Palestina" huko Gaza. Alimwambia mshirika wake, Marekani, pamoja na Hamas kwamba haiko tayari kwa uhuru wa Palestina.

■ Wakati Umoja wa Ulaya ukituma ishara zinazokinzana kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, kwa kuiwekea vikwazo Hamas pia kwa kutoa shutuma dhidi ya Israel, mkutano utafanyika Jumatatu hii mjini Brussels na mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya na wenzao sita katika eneo hilo.

■ Hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza "haiwezi kuwa mbaya zaidi", ametangaza leo Jumatatu Mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell. "Kuanzia sasa, sitazungumza tena kuhusu mchakato wa amani, lakini nataka mchakato wa ufumbuzi wa serikali mbili," Bw. Borrell amesema.

■ Kulingana na ripoti iliyotangazwa siku ya Jumapili Januari 21 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 25,105 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Zaidi ya watu 62,681 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.