Pata taarifa kuu

Hamas yakataa 'mradi wowote wa kimataifa au wa Israel kuhusu mustakabali wa Ukanda wa Gaza'

Kundi la Hamas siku ya Jumapili limetaka "uchokozi wa Israel" katika Ukanda wa Gaza usitishwe mara moja , na kutangaza kwamba watu wa Palestina pekee ndio wanapaswa kuamua mustakabali wa Gaza.

Wagonjwa wa Kipalestina wakiwa wameketi kweye vitanda vyao ndani ya meli ya kijeshi ya Ufaransa “LHD Dixmude”, kwenye bandari ya Misri ya el-Arich Jumapili hii, Januari 21, 2024.
Wagonjwa wa Kipalestina wakiwa wameketi kweye vitanda vyao ndani ya meli ya kijeshi ya Ufaransa “LHD Dixmude”, kwenye bandari ya Misri ya el-Arich Jumapili hii, Januari 21, 2024. AFP - KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

 

"Tunakataa kabisa mradi wowote wa kimataifa au wa Israel unaolenga kuamua mustakabali wa Ukanda wa Gaza," Hamas imeandika katika waraka wa maelezo pia ikirejelea mashambulizi yake yaliyotekelezwa Oktoba 7 katika ardhi ya Israel.

Katika waraka huo, Hamas inazingatia kwamba shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israeli lilikuwa "hatua ya lazima" na "jibu la kawaida" kwa "njama zote za Israeli dhidi ya watu wa Palestina." Kulingana na Hamas, katika "machafuko" karibu na mpaka kati ya Israel na Ukanda wa Gaza, "labda makosa yalifanyika", lakini kundi hilo linakanusha kuwa lililenga raia, isipokuwa "kwa bahati mbaya, na wakati wa makabiliano na vikosi vya wavamizi."

Watu elfu moja mia moja na arobaini waliuawa, kulingana na shirika la habari la AFP, wakati wa shambulio hili ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini Israeli. Wengi walikuwa raia, kulingana na hesabu za AFP likinukuu data rasmi ya Israeli, ikiwa ni pamoja na zaidi ya wahudhuriaji 360 wa tamasha huko Reim.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.