Pata taarifa kuu

Israel: Wakimbizi kutoka kaskazini mwa Gaza wanaweza kurejea 'wakati hakuna hatari tena'

Jeshi la Israel limesema litafikiria kuruhusu kurejea kwa raia wa Kipalestina waliokimbia makazi yao kutoka kaskazini mwa Ukanda wa Gaza wakati litakapoamua kuwa hawatakuwa katika hatari yoyote kufuatia mapigano na Hamas.

Katika kambi huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 10, 2024.
Katika kambi huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 10, 2024. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Herzi Halevi amewaambia waandishi wa habari: "Tunapojua kuwa hakuna hatari tena kwa raia, tunaweza kufikiria kuwarudisha makwao."

Vikosi vya Quds vinasema vvyarusha risasi kuelekea Kibbutz Erez

Katika taarifa, tawi la kijeshi la Islamic Jihad kutoka Palestina, limedai kushambulia Erez na "makaazi ya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza" kwa safu ya makombora, kulingana na Al-Jazeera. Saa moja kabla, Gazeti la Haarezt lilitangaza kuwa karibu na Gaza kengele zilikuwa zikisikika kuonya kuhusu kurushwa kwa roketi.

Hezbollah yadai kukipiga kijiji cha Israeli, kulingana na al-Jazeera

Kundi la Lebanon linadai kushambulia kijiji cha Shtula, karibu na mpaka wa Lebanon, na kuharibu moja ya majengo yake. Katika taarifa kupitia kituo chake cha Telegram, Hezbollah imesema shambulio lake dhidi ya jengo la kiraia lilikuwa jibu kwa "mashambulizi ya Israeli dhidi ya nyumba na vijiji vya kusini, shambulio la hivi karibuni zaidi likiwa ni shambulio la anga dhidi ya mji wa Yarin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.