Pata taarifa kuu

Gaza yakabiliwa na mashambulizi ya jeshi la Israel huku mzozo ukienea hadi Yemen

Jeshi la Israel linaendelea na operesheni zake katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumamosi, Januari 13, unaokabiliwa n akukatika tena kwa mawasiliano ya simu, huku vita kati ya Israel na Hamas vikihamia tangu Ijumaa kwa sehemu hadi nchini Yemen, ambako majeshi ya Marekani na Uingereza yalifanya hivi karibuni mashambulizi dhidi ya Israel. Waasi wa Houthi wa Yemen wanatishia usafiri wa meli katika Bahari Nyekundu.

Mlipuko wa bomu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 13, 2024.
Mlipuko wa bomu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Januari 13, 2024. © AMIR COHEN / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi mapya Jumamosi dhidi ya maeneo ya waasi wa Houthi nchini Yemen baada ya waasi hao kuongeza vitisho vyao dhidi ya usafiri wa kimataifa bahari katika Bahari Nyekundu. Mapema siku ya Ijumaa, mashambulizi ya Marekani na Uingereza yalilenga maeneo ya kijeshi yanayoshikiliwa na Wahouthi.

■ Siku ya Jumamosi, milipuko ya mabomu imeendelea huko Gaza, kulingana na shirika la habari la AFP. Siku hiyo, mashambulizi ya Israel pia yalilenga kusini mwa Lebanon dhidi ya Hezbollah, linathibitisha jeshi la Israel. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa unalishutumu jeshi la Israeli kwa kupunguza usambazaji wa mafuta, hasa kwa hospitali. Huduma za mawasiliano zimekatizwa kabisa.

■ Kulingana na ripoti iliyotolewa siku yaumamosi hii, Januari 13 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 23,843 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 60,000 wamejeruhiwa. Baada ya siku 99 za vita huko Gaza, zaidi ya watoto 10,000 - au 1% ya jumla ya watoto wa Ukanda wa Gaza - wameuawa, kulingana na ripoti mpya kutoka shirika la Save The Children.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.