Pata taarifa kuu

Ripoti: Asilimia moja ya watoto wameuawa katika Ukanda wa Gaza

Baada ya takriban siku 100 za vita huko Gaza, zaidi ya watoto 10,000 - au 1% ya jumla ya watoto wote wa Ukanda wa Gaza - wameuawa, kulingana na ripoti mpya kutoka shirika ka Save The Children. Watoto walionusurika vitani "huvumilia mambo ya kutisha yasiyoweza kuelezeka, hususan majeraha yanayobadilisha maisha, kuchomwa moto, magonjwa, kutopata matibabu ya kutosha, na kufiwa na wazazi wao na wapendwa wengine," ripoti hiyo imesema. 

Huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza. AFP - MAHMUD HAMS
Matangazo ya kibiashara

Kati ya maelfu ya watoto waliojeruhiwa, angalau 1,000 walipoteza mguu mmoja au yote miwili, kulingana na ripoti hiyo. Kila siku tangu kuanza kwa vita hivyo, zaidi ya watoto kumi wamepoteza angalau mguu mmoja au yote miwili, wengi walikatwa viungo hivyo bila kupigwa ganzi. 

"Idadi hiyo sio tu ya kushangaza katika ukubwa na upeo wao, lakini pia katika athari zao halisi," Jason Lee kutoka shirika hilo lisilo la kiserikali la ameiambia Al Jazeera. "Sio takwimu tu. Kila mmoja wao ni mtoto."

Wakati huo huo Israel inatarajia kujibu Ijumaa hii, Januari 12, kwa kile nchi hiyo inachoeleza kuwa ni madai ya "kinyama" kwamba inafanya "mauaji ya halaiki" huko Gaza, katika kesi ya kihistoria ya kisheria mbele ya mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa. Hayo yanajiri wakati, mashambulizi ya anga yanaendelea katika Ukanda wa Gaza, pia kuwapiga watoto, na hali ya wasiwasi inaongezeka katika Bahari Nyekundu. Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen, ambao katika wiki za hivi karibuni waliongeza mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu katika "mshikamano" na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Siku ya Alhamisi Afrika Kusini iliomba Mahakama ya Dunia kuamuru Israel isitishe mara moja operesheni yake ya kijeshi huko Gaza, ambapo inadai kuwa Israel ina "nia ya mauaji ya kimbari" dhidi ya raia wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.