Pata taarifa kuu

Iran: Milipuko miwili yaua watu zaidi ya 100 karibu na kaburi la Qassem Soleimani

Takriban watu 103 wameuawa na 180 kujeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea Jumatano Januari 3 huko Kerman (kusini-mashariki), ambapo hafla ilikuwa ikifanyika kwa kumbukumbu ya mkuu wa zamani wa kikosi cha al-Quds, Qassem Souleimani. Milipuko hiyo miwili imeelezewa kama "shambulio la kigaidi" na televisheni ya Irani. Tehran imetangaza siku ya Alhamisi kuwa siku ya maombolezo. Rais wa Iran ameaani shambulizi "mbaya". Ayatullah Khamenei ameahidi "jibu kali". EU imelaani "kitendo cha kigaidi".

Mtu aliyejeruhiwa akipokea msaada baada ya milipuko miwili iliyofuatana ikilenga umati wa watu waliokuwa wakiadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani alyeuawa mnamo mwaka 2020. Tukio hilo lilitokea karibu na msikiti wa Saheb al-Zaman katika mji wa kusini wa Kerman nchini Iran, Januari 3, 2024.
Mtu aliyejeruhiwa akipokea msaada baada ya milipuko miwili iliyofuatana ikilenga umati wa watu waliokuwa wakiadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani alyeuawa mnamo mwaka 2020. Tukio hilo lilitokea karibu na msikiti wa Saheb al-Zaman katika mji wa kusini wa Kerman nchini Iran, Januari 3, 2024. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi amelaani siku ya Jumatano shambulizi ambalo limeua takriban watu 103, karibu na kaburi la mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi Qassem Soleimani aliyeuawa mnamo mwaka 2020, na kukemea kitendo "kiovu" na cha "aibu". "Hakuna shaka kwamba wahusika wa kitendo hiki kiovu hivi karibuni watatambuliwa na kuadhibiwa kwa kitendo chao cha kinyama, na vikosi vya usalama na vikosi vyenye taaluma," Bw. Raïssi amesema katika taarifa.

Kwa upande wake, Ayatollah Khamenei ameahidi "jibu kali". "Maadui waovu na wahalifu wa taifa la Iran kwa mara nyingine tena wamesababisha maafa na kugeuza idadi kubwa ya watu wetu huko Kerman kuwa mashahidi," Kiongozi Mkuu Ali Khamenei amesema katika taarifa. "Janga hili litajibiwa vikali, Mungu akipenda," ameongeza.

Milipuko miwili imetokea, televisheni ya serikali imeripoti. Mlipuko wa kwanza ulisikika karibu na msikiti wa Saheb al-Zaman, ambapo kaburi la Qassem Soleimani linapatikana, huko Kerman, mji wa nyumbani kwake, kusini mashariki mwa Iran, televisheni ya taifa imetangaza, kabla ya kuongeza kuwa mlipuko mwingine ulisikika dakika chache baadaye. "Tukio hilo ni shambulio la kigaidi," vyombo hivyo vya habari vimesema, vikimnukuu Rahman Jalali, naibu gavana wa jimbo la Kerman, kusini mwa Iran.

Idadi ya vifo imeendelea kuongezeka kila baada ya saa, anaripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi. Waziri wa Mambo ya Ndani amezungumza hivi punde kwenye televisheni ya Iran: anasema Iranimeapa kulipiza kisasi bila kujali. Hata hivyo, hakushutumu kundi au taifa lolote, hasa Israel, lakini maafisa wengine wameanza kudai kuwa taifa la Kiyahudi ndilo limehusika na mashambulizi hayo mawili.

Mashambulizi haya mawili yanakuja siku chache baada ya kuuawa kwa kamanda mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi wakati wa shambulio la anga la Israeli huko Damascus, hali ambayo bila shaka itazidisha hali ya vurugu katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu yaliyofichwa kwenye mifuko miwili, mabomu ambayo yanaonekana kuwashwa na rimoti. Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha washiriki wakijaribu kuondoka kwenye eneo la tukio baada ya milipuko hiyo, huku maafisa wa usalama wakizingira eneo hilo. Wafanyakazi wa shirika la habari la Hilali Nyekundu walifika haraka kwenye eneo la tukio kuwahudumia majeruhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.